Chabo Zamkimbiza Davina

Chabo Zamkimbiza Davina
MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Halima Yahaya ‘Davina’ amejikuta akitoka nduki baada ya kushtukia anapigwa chabo na makonda wa daladala.

Tukio hilo la aina yake lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Ubungo- Mawasiliano wakati Davina na wenzake wakiwa wanarekodi sinema inayokwenda kwa jina la Kashinde ya inayoandaliwa na Kampuni ya Lugwa.

Wakati akibadilisha nguo kuuvaa uhusika wa ‘ukonda’ nyuma ya gari, ghafla walitokea makonda halisi ambao walimfanya atimke haraka akihofia kuchunguliwa.

“Daah! Kazi yetu hii ina changamoto wakati mwingine inabidi ujitoe kidogo ufahamu lakini pale niliamini hakuna mtu angeweza kufika sijui wale makonda walitokea wapi,” alisema Davina.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad