Chadema Nao Wasimamisha Kampeni za Uchaguzi wa Marudio

Chadema Nao Wasimamisha Kampeni za Uchaguzi wa Marudio
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo Februari 5, 2018 kimesimamisha kampeni za uchaguzi wa marudio ili kushiriki shughuli ya maziko ya Mwanasiasa mkongwe Kingunge aliyefariki dunia Februari 2, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)


Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amesema hayo leo na kuwakaribisha wanachama mbalimbali wa CHADEMA kushiriki katika mazishi ya kiongozi huyo

"Kwa heshima ya Mzee wetu Kingunge, leo Jumatatu 05/02/2018 CHADEMA haitafanya mikutano ya kampeni ili kushiriki shughuli ya maziko ya baba yetu, mpiganaji aliyechagua kuyapigania bila woga mabadiliko ya kweli hapa nchini. Tutatoa heshima za mwisho na kuuaga mwili wa Kingunge Karimjee na baadae kwenye kumpumzisha Mzee wetu kwenye makaburi ya Kinondoni" alisema Mbowe

"Wananachama wa CHADEMA, wapenzi, mashabiki na wananchi wote kwa ujumla mnakaribishwa kumsindikiza baba yetu katika safari yake ya mwisho"

Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, Amina.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad