Chadema Yadai Hawana Imani na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni

Chadema Yadai Hawana Imani na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo wamesema hawana imani na msimamizi wa uchaguzi jimbola Kinondoni wakidai kuna njama zilizopangwa dhidi ya chama hicho katika uchaguzi utakaofanyika wiki ijayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa Chadema, Benson Kigaila,  amesema baadhi ya njama hizo ni kuwepo taarifa kwamba kuna watu walioletwa kutoka Zanzibar kuja kushiriki uchaguzi huo wa Kinondoni ambapo amesema wapo kwenye hoteli na nyumba za kulala wageni eneo la Kijitonyama, Kinondoni,  jijini Dar es Salaam.

Kigaila aliongeza kusemakwamba chama chake kimeona dalili za hujuma ambazo hupangwa kila unapofika wakati wa uchaguzi  ambapo watu hushambuliwa, kutekwa na kufanyiwa vitendo vibaya.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad