Chirwa Afunguka Kuhusu Msimamo Wake Yanga

Chirwa Afunguka Kuhusu Msimamo Wake Yanga
BAADA ya kuwepo kwa taarifa mbalimbali zikimhusu straika wa Yanga, Obrey Chirwa raia wa Zambia kugoma kuichezea timu hiyo, mwenyewe ameibuka na kutoa msimamo wake ndani ya timu hiyo.

Chirwa aliyejiunga na Yanga msimu uliopita akitokea FC Plati­num ya Zimbabwe, mkataba wake na Yanga unatarajiwa kumal­izika mwishoni mwa msimu huu huku kukiwa na taarifa za Simba kuinyemelea saini yake.

Hivi karibuni, taarifa zilitoka zikidai kwamba, Mzambia huyo ametaka kupewa kitita cha shilingi milioni 150 ili aongeze mkataba ndani ya timu hiyo.

Taarifa za Chirwa kugoma kuichezea Yanga, zilianza wik­iendi iliyopita baada ya jina lake kuondolewa dakika za mwisho kwenye msafara wa timu hiyo ulioelekea Shelisheli kucheza mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St Louis.

Katika mch­ezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar, Yanga iliibu­ka na ushindi wa bao 1-0, ambapo kwenye mchezo huo, Chirwa alikosa pen­alti, huku Yanga ikifunga bao lake hilo kupitia kwa Juma Mahadhi.

Kuachwa kwa Chirwa kwenye msafara huo, kulitolewa ufafanuzi na Yanga kwa kusema kuwa, mchezaJi huyo alipata majeraha kwenye mch­ezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Majimaji ambao Yanga walishinda mabao 4-1.

Baada ya kuenea taarifa za kugoma kwa Chirwa, juzi Ju­matatu klabu hiyo iliweka katika akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram sehemu ya mahojiano na Chirwa.

“Sijawahi kusema wala kumwambia mtu yeyote kuwa nataka 150M kwa ajili ya mkataba mpya, sipendezwi na namna wanavyoni­zushia, nadhani nia yao ni kunigombanisha na wapenzi wa Yanga.

“Niliumia kwenye mchezo dhidi ya Maji­maji, ajabu wanasema nimegoma, huu ni upu­uzi, mimi ni mchezaji wa Yanga, mimi na klabu ndiyo wenye kujua hati­ma yangu ya baadaye, niacheni nicheze mpira,” alisema Chirwa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad