Damu ya Msanii Radio Yazidi Kufanya Kazi ...... Polisi Yamsaka Producer Washington Ambaye Amehusishwa Kifo cha

Damu ya Msanii Radio Yazidi Kufanya Kazi ...... Polisi Yamsaka Producer  Washington Ambaye Amehusishwa Kifo cha
Jeshi la Polisi nchini Uganda leo linakusudia kumkamata producer wa muziki nchini Uganda maarufu kwa jina la Washington, ambaye amehusishwa na kifo cha msanii Radio.


Kwa mujibu wa msemaji wa kundi hilo amesema Washington ndiye mtu aliyemchukua Radio kutoka nyumbani na kwenda naye club ambako alipigwa hadi kupelekea kifo chake, kutokana na kutoa maelezo yasiyoeleweka.

“Tunaenda kumkamata Washington leo, Washington ndiye alimchukua Radio na kwenda naye mahali ambako aliuawa, kutokana na maelezo anayoyatoa kuwa ya kuchanganya yasiyoeleweka”, amesema msemaji huyo.

Pia Polisi wa Uganda tayari wamemkamata mtu aliyempiga Radio hadi kupekea kifo chake anayejulikana kwa jina la Troy, ambaye ametajwa na producer Washington aliyekuwa naye siku ya tukio mpaka anapigwa.

Mpaka Radio anakutwa na umauti Troy alikuwa amejificha kwenye nyumba ya rafiki yake iliyopo Entebe Uganda.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad