Familia ya Akwilina Yatoa Onyo kwa Wanaochangisha Fedha za Msiba Mitandaoni

Familia ya Akwilina Yatoa Onyo kwa Wanaochangisha Fedha za Msiba Mitandaoni

Familia ya mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyeuawa kwa kupigwa risasi Februari 16, 2018  imewaonya watu wanaochangisha fedha za msiba wa mwanafunzi huyo mitandaoni.

Imesema inawafuatilia wanaofanya hivyo kutokana na kuibuka kwa tetesi kuwa michango hiyo inachangishwa kinyume na utaratibu kupitia mitandao mbalimbali.

Msemaji wa familia, Festo Kavishe leo Februari 20, 2018 amewaalika ndugu jamaa na marafiki kufika Moshi Hoteli saa 11 jioni kwa ajili ya michango ya msiba.

"Hatutaki wananchi wapitishe michango yao kwa njia ya simu kwa sababu matapeli wapo wengi sasa hivi, ukipata meseji ya kuombwa mchango fikisha nyumbani,” amesema Kavishe.

"Hata taasisi mbali mbali zinakuja kwa ajili ya kutupa pole  inasaidia katika msiba huu. Njia rahisi ya kuchangia msiba huo ni kufika nyumbani kwa dada yake Akwilina kufikisha mchango wako na sio kwa njia ya simu."
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad