Yupo mwanahabari mmoja jana aliandika makala isemayo ufungeni Uwanja wa Taifa,kwenye andishi lake liliojaa makosa makubwa ya kalamu na tanahui za kiuandishi,mwandishi huyo licha ya upotofu mkubwa aliuofanya juu ya matumizi ya Uwanja wa Taifa pia alinilisha maneno ya uongo juu ya kauli yangu kuhusu mchezo wa kesho baina ya Yanga na timu toka Shelisheli.
Najua kwa kumjibu kwangu itampa umaarufu ambao siku hizi unaitwa kiki,lakini kumuacha itakuwa anadhani mm au wanasimba wanamuogopa kwa kuwa anafanya kazi ya utangazaji kwenye moja ya vituo vya Televisheni vinavyoheshimika nchini.
Kwa hili la Yanga kutoruhusiwa kuutumia Uwanja Mkuu wa Taifa na kulaumu wamiliki wa uwanja ambao ni Serikali ni wajibu wangu kama mdau wa Soka kumhabarisha huyu jamaa anaependa kutumia lahaja za kikwaya kwaya na kingonjera ktk utangazaji kwamba,hakuna mahali kokote na nchi yoyote Afrika kwa klabu ya Tanzania au Timu ya Taifa ilipozuiwa kutumia uwanja utakaotumika siku ya mchezo ikiwa ugenini.
Hiyo ni kanuni ya FIFA na CAF na haina mjadala wa matumizi yake,kwake yeye anadhani kwa Washelisheli kuruhusiwa kuutumia Uwanja wa Taifa leo ni kuwapendelea,laa hasha!ni kanuni ndizo zinazotaka timu ngeni kutumia uwanja utakaotumika kwa ajili ya mchezo siku moja kabla ya mechi yenyewe.
Pia kwenye makala yake ameelezea kusikitishwa kwake na Yanga kutoruhusiwa kuutumia Uwanja wa Taifa kwa mazoezi wakati huu ikijiandaa kwa ajili ya mchezo huo,huku akiishutumu wamiliki kuwa wanataka kuugeuza uwanja huo kwa mambo ya kisiasa..hakuishia hapo mpiga zumari huyo akawalaumu na walioukarabati uwanja utaalamu wao ni wa kutiliwa mashaka kwa kupanga matumizi ya Uwanja huo wa kisasa kabisa.
Na akahoji mbona vwanja vkubwa Afrika na Ulaya vinatumika kila siku akimaanisha hata kwa mazoezi? Laa haulaaaa!!! Jamaa hajui kisha anajiona anajua..nimpe elimu ndogo tu ya ufahamu kwake na kwa wingine,, hakuna vilabu vinavyotumia hvyo alivyoviita vwanja vikubwa kwa mazoezi..mazoezi kwenye hvyo vwanja hutumiwa na timu ngeni siku moja kabla ya mchezo,narudia ni timu ngeni tena siku ya kuamkia mchezo.
Klabu zote hutumia vwanja vyake vya mazoezi kwa maandalizi yake ya mechi na sio kukaa kulaumu Serikali na waliovikarabati kampuni ya Spotipesa huku hujui nn unaandika.
Kujitia uzalendo pori kwa kulaumu jambo la kikanuni ni kujitia hamnazo kusudi, kwangu mm uzalendo ungekuwa kutuhimiza Simba na Yanga tuwe na vwanja vyetu wenyewe kwa ajili ya mazoezi,Simba tuanze haraka mradi wa Bunju na kwa Yanga shime iendelee ya kujaza vifusi pale Jangwani.
Mtangazaji huyu ambae hutumia sanaa ya majukwaani ktk kazi yake pia alinilaumu mm na kunilisha maneno eti nimewataka washabiki wetu wakaishangilie Yanga kwenye mchezo wake wa kesho na akadai nafanya propaganda ili kuwahadaa wanayanga.
Kwanza mm sikusema washabiki wetu wakaishangilie Yanga.. nilichosema na kutoa rai yangu tuachane na utamaduni wa kuzomeana inapokuja ishu ya kuwakilisha nchi,kwangu mm huo c utamaduni wa kishabiki kokote ulimwenguni,hauwezi kuukuta nchi yoyote hata zile zenye ushabiki uliokubuhu wa mpira,iwe Spain,Misri,Uturuki na hata Tunisia.
Mcheza sanaa huyu alienda mbali zaid kwa kudai eti nimesema hvyo kwa kuwa najua Yanga watashinda kesho,hvyo ninawahadaa,uhh lalaaa! Sijui ni aina gani ya mwandishi anayejipambanua hadharani mahaba yake hadharani kwa klabu moja,Na kwa kufanya hvyo sijui atapataje legitimacy ya kupata stori toka kwetu!!!
Kauli hyo ilipaswa itolewe na uongozi wa Yanga lakini pia wao hawawezi sababu mm nimeongea na washabiki wetu ambao mm ni msemaji wao.
Inaonekana jamaa ana chuki zake na Simba na ndio maana mara nyingi amekuwa akitushambulia bila sababu, makala yake ya mwisho huku akitumia tafsida ya waimba Taarabu,alimtahadharisha kocha wetu mpya kwa mafumbo yanayotumiwa majumbani kwa kebehi kubwa sana..
Nilikaa kimya sababu hang'ati, yaani hana sumu, lakini kwa hili nimeamua kumjibu sababu uongo ukiachwa sana huaminika na mm nimejiapiza nikiwa msemaji wa klabu hii kubwa kabisa nchini,sitaacha klabu yangu ishutumiwe kwa mambo ya uongo na ya kuzua toka kwa yoyote yule,wajibu wangu mwingine klabuni ni kuitetea na kulinda Image na brand ya Simba.
Sina maana kuwa kila tufanyalo ni sahihi,au nnazuia kukosolewa,Hapana....maana yangu tukosolewa tunapostahili tena kwa heshma,hii ni klabu ya Watu sio klabu ya kijiweni....
Ijumaa kareem...