Halima Mdee Aliamsha Dude Bungeni Awavuruga Mawaziri

Halima Mdee Aliamsha Dude Bungeni Awavuruga Mawaziri
Naibu Waziri wa Afya,  Dkt. Ndugulile leo Februari 1, 2018 amefunguka na kusema Serikali haijazuia wanafunzi wa kike kutoendelea na masomo baada ya kupata ujauzito bali ilizuia mwanafunzi kurudi shule aliyokuwa akisoma awali kabla ya kupata ujauzito.

 Ndugulile amesema hayo leo Bungeni wakati akijibu swali ambalo liliulizwa na Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya CHADEMA, Halima Mdee ambaye alitaka kujua juu ya utekelezaji wa sera ya 're entry policy' ambayo ilianzishwa katika kipindi cha awamu ya nne ya Serikali kuwawezesha wanafunzi waliopata ujauzito kurudi shule baada ya kujifungua kupata haki yao ya kimsingi ya kusoma.

Akijibu swali hilo Ndugulile alisema kuwa "Ni kweli kulikuwa na maandalizi ya 're entry policy' lakini utekelezaji wake sasa umepitwa na wakati kutokana na agizo lililotolewa na Serikali kwamba mtoto ambaye amepata ujauzito hataruhusiwa kurudi katika shule ambayo alikuwa anasoma lakini maagizo haya hayajazuia mtoto wa kike ambaye amepata ujauzito kutoendelea na masomo hapo naomba tuelewane vizuri. Serikali imezuia mtoto wa kike kurudi shule aliyokuwa akisoma ila haijazuia mtoto wa kike kuendelea na masomo" alisema Ndugulile

Mbali na hilo Naibu Waziri huyo amesema kuwa sasa Serikali inaangalia njia mbadala ambayo itawawezesha watoto wa kike ambao wamepata ujauzito ili waweze kuendelea na masomo.

Baada ya kauli ya Naibu Waziri aliibuka Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa. Joyce Ndalichako na kuweka msimamo wa Serikali kuwa mwanafunzi ambaye amepata ujauzito hawezi kurudi shule kama ambavyo Naibu Waziri wa Afya amesema.

Mwezi June 23, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alisema serikali yake haitoruhusu mwanafunzi aliyepata ujauzito kuendelea na masomo.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jamani na mm naomba serikali ingiilie kati swala la wananchi kuzuiliwa airport mimi niliingia tarehe 25 January kumrudisha mtoto kutoka Dubai tarehe 26 wakati narudi nimezuiliwa airport na nina kilakitu cha halali Mimi najishughulisha na hoteli Nina mkataba,ninakibali na icho kibali nililipia laki 4 mbili ubalozi Wa Dubai 2 nimelipa tewasa na hata miezi 3 bado toka nilipie na Nina visa ya miaka 3 lakini cha ajabu watu wanakuzuia kusafiri je iyo ni haki ticket yangu imekwenda bure na kz nimepoteza haki ipo wapi Tanzania tunaenda wapi tutafika kweli.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad