Hii Hapa Ratiba Mpya ya Simba na Yanga

Hii Hapa Ratiba Mpya ya Simba na Yanga
Shirikisho la soka nchini limebadili tena ratiba ya ligi kuu soka Tanzania Bara mara hii ikihusisha michezo ya timu za Simba na Yanga kusogezwa mbele na mwingine kurudisha nyuma.


Kwa upande wa mchezo wa Simba SC dhidi ya Stand United uliotakiwa kuchezwa jumapili ya Februari 4, umerudishwa nyuma kwa siku mbili hadi Ijumaa Februari 2, ukipigwa katika uwanja wa taifa Dar es salaam.

Mchezo huo umerudishwa nyuma ili kuipa nafasi klabu ya Simba kujiandaa na mchezo wake wa hatua ya kwanza kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry ya Misri utakaopigwa Februari 7.

Kwa upande wa Yanga mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar uliokuwa uchezwe Februari 3 kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro umepelekwa mbele na tarehe yake itatajwa hapo baadae.

Simba inaongoza ligi ikiwa na alama 45 kwenye mechi 19, huku wapinzani wao Yanga wakiwa katika nafasi ya pili na alama 37 kwenye michezo 18. Yanga kesho itakuwa ugenini kucheza na Ndanda FC kwenye mchezo wa ligi kuu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad