Hizi Hapa Sababu Zinazofanya Wanawake Kupata Ukimwi Zaidi ya Wanaume

Hizi Hapa Sababu Zinazofanya Wanawake Kupata Ukimwi Zaidi ya Wanaume
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulile leo Februari 9, 2018 ameweka wazi sababu nne ambazo zinapelekea wanawake wengi zaidi kuonekana wanapata maambukizi ya UKIMWI ukilinganisha na wanaume.


Ndugulile amesema hayo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtambwe (CUF), Khalifa Mohamed Issa ambaye alitaka kufahamu sababu za kitaalam zilizopelekea idadi kubwa ya wanawake kuwa ndio waathirika wa virusi vya UKIMWI kuliko wanaume. Akijibu swali hilo Ndugulile alikiri kuwepo kwa sababu nne.

"Sababu za kitaalam zinazosababisha wanawake wengi kuathirika zaidi na maambukizi ya VVU na UKIMWI yapo kama manne moja ni sababu ya kimaumbile na kibaolojia, mwanamke yupo katika hatari zaidi ya kupata VVU ukilinganisha na wanaume kwa kuwa maumbile ya mwanamke ni rahisi kupata michubuko wakati wa tendo la ndoa na hivyo kurahisisha virusi vya UKIMWI kupenya aidha maumbile ya mwanamke hupokea mbegu za kiume kutoka kwa wanaume wakati wa tendo la ndoa iwapo mwanamke atafanya mapenzi na mwanaume mwenye VVU mwanamke huyo anaweza kuambukizwa maambukizi ya UKIMWI"

Naibu Waziri wa Afya aliendelea kutoa ufafanuzi kuwa

"Sababu ya pili kwamba kuna tabia na mazingira hatarishi ambayo husababisha hatari zaidi kwa wanawake kuambukizwa VVU ikiwa ni pamoja na kufanya biashara ya ngono na kuanza mapenzi katika umri mdogo, lakini sababu ya tatu ni mfume dume uliokuwepo katika jamii yetu unawapa fursa wanaume ya kuamua kufanya ngono na wanawake wengi, kutotumia kondom, kuoa wasichana wenye umri mdogo na hata kufanya ukatili wa kijinsia. Mfumo huu unasababisha wanawake kuambukizwa VVU na hata kushindwa kueleza ukweli kwa wenza wao kuhofia kuachika, kutengwa au kufukuzwa katika familia"

"Sababu ya mwisho ni kwamba wanawake wengi hujitokeza kupima kuliko wanaume hivyo nitoe rai kwa wanaume kujitokeza kupima tusitumie wenza wetu kama kipimo cha maambukizi yetu sisi" alisisitiza Ndugulile

Inakisiwa kuwa kwa Tanzania idadi ya watu wote wanaoishi na virusi vya UKIMWI imefikia milioni moja laki tano huku idadi ya wanawake ikiwa kubwa zaidi kulinganisha na wanaume.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad