Huyu Hapa Ndiye Mwanafunzi Aliyepigwa Risasi na Polisi Wakati wa Maandamano ya CHADEMA


Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) imepokea kwa mshituko taarifa za kifo cha mwanafunzi Aqulina Akwilini ambaye inasemekana amepigwa risasi na polisi wakati wakikabiliana na waandamanaji wa Chadema jana.Awali taarifa hizo zilimhusisha mwanafunzi huyo na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) lakini baada ya uchunguzi wa kina imebainika ni mwanafunzi anayesoma Chuo cha Usafirishaji NIT

R.I.P

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Inasikitisha lakini inaonekana viongozi wa Chadema wamepata kile walichokuwa wakikitafuta ni kuanzisha vurugu katika uchaguzi huo mdogo wa kinondoni baada ya kuona hawana uwezo wa kushinda uchaguzi huo. Lengo kubwa la Chadema la kuanzisha vurugu ni kuja kutoa visingizio yakwamba uchaguzi ulikuwa si wahuru na haki itakapotokea kushindwa uchaguzi. Tanzania ni nchi yenye vyombo vya sheria kama vile Mahakama kwanini viongozi wa Chadema wasifuate taratibu za kimahakama kuwakilisha madai Na malalamiko yao na badala yake huamua kujichukulia sheria mikononi mwao pamoja na kuwashawishi wafuasi wao kuvunja sheria za nchi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usiongee kama sio binadamu wewe. Una watoto wewe? Hivi mnafanya ukatili wa namna hii in the name ya siasa haafu hapa unajaribu kupoteza ukweli na kujidai kuilaumu chadema? unafikiri Mungu haoini au? Hayo madaraka mnayotaka kuwa nayo milele mtaenda nayo wapi? Haya kwani ni mauaji ya kwanza? umeshafikiri kuhusu watu wote wanaouwawa? unafikiri watu wote ni wajinga kuamini upuuzi unaoongea? msichana mdogo kama yule kuuwwa kinyama namna hii halafu uko hapa unaonge utumbo. Kama mama ninasikia uchungu sana. Mpaka mtoto wako au mwenyewe utakapoathirika na haya mambo ndio akili itakukaa sawa. kwa nini wtanzania mnajifanya vipofu kuona ukatili huu unaofanywa bila haya? huu ni ukatili wa watu wachache ambao hawataki kuachia madaraka kwa wengine hata kama ikibidi damu imwagike. kwani aliyekwambia kwamba ccm ndiyo lazima itawale nani? kwani nchi si ya watu wote? ujinga huu mpaka lini kuona kwamba wengine wanastahili na wengine hawastahili? mtaua watu sana lakini hizi damu siku moja zitawarudia. Hakuna excuse hapo. Matendo yote ya ukatili wanayofanyiwa watu ili chama kibaki madarakani siku Moja Mungu Atajibu na akijibu atajibu kwa tetemeko. Mwogopeni Mungu hao watu mnaowaua ili mbaki madarakani nao ni binadamu. Mungu atawaumbua siku moja maana biblia inasema linalofanyika sirini Mungu ataliweka wazi. Usijifanye unajua sana kutufanya wote wajinga eti tuwalaumu chadema. Kwa hili serikali na chama kilichopo madarakani vinahusika moja kwa moja na Mungu aliye juu atawashuhulikia tu. Auae kwa upanga atakufa kwa upanga.

      Delete
  2. Kwani nani alieitisha maandamano? CCM?
    Chadema ni chama cha vurugu hakuna asiejua. Chadema ni chama cha hovyo na hasa tangu aondoke Dr Slaa Chadema kimekuwa chama cha hovyo zaidi kazi kubwa ni kuhamasisha ukabila na udini katika siasa. Masikini msichana yule alikuwa na dreams zake lakini kaenda kukatana na watu wa hovyo wakamtoa kwenye mwelekeo. Ni ugonjwa wa akili kwa Chadema kujifanananisha na CCM kiupinzani. Kwa CCM hii ya Magufuli Chadema wataishia kuwadanganya wafuasi wao kuwa wanadhulumiwa ndio maana wanashindwa uchaguzi lakini ukweli ni kwamba CCM ni maji yenye kina kirefu Chadema kujaribu kwenda kuogelea kwa sasa watazama tu.

    ReplyDelete
  3. Isingekuwa Mbowe na hemge lake leo binti yetu anhekuwa hai na angelijenga Taifa siki za.mbele

    Mbowe amesababisha hili tukio na he has to pay it.
    kwanza kwa Mungu pili kwa familia ya wafiwa tatu kwa taifa kutiondolea Damu mbichi iliyokuwa na mustakbali.
    Mbowe na genhe lako ni lazima sheria iwachukulie hatua stahiki kusababisha hili kifo cha mtoto asie na hatia.

    ReplyDelete
  4. The price of MP position under .......


    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad