Ibada ya Kumuombea Kingunge Yafanyika Nyumbani Kwake

Ibada ya Kumuombea Kingunge Yafanyika Nyumbani Kwake
Ibada ya kumuombea  mwanasiasa mkongwe marehemu Kingunge Ngombale Mwiru imefanyika nyumbani kwake Victoria, Kijitonyama wilayani Kinondoni.

Ibada imefanyika leo Jumatatu Februari 5,2018 ikiongozwa na katekista George Wilbard wa Kanisa Katoliki.

Baada ya ibada, mwili wa Kingunge utapelekwa katika viwanja vya Karimjee  kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho.

Kingunge aliyefariki dunia Februari 2,2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kung’atwa na mbwa nyumbani kwake atazikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad