Sirro amesema hayo Februari 26, 2018 akiwa Bariadi Mkoani Simiyu wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ambapo amedai kuwa amekuwa akiona kuna watu kupitia mitandao ya kijamii wamekuwa wakihamasisha watu kufanya maandamano.
"Wote tunajua kwamba maandamano Katiba imetamka na sheria za vyama vya siasa imetamka kwamba maandamano ni haki kwa raia lakini kuna utaratibu wa maandamano, sasa kuna maandamano ambayo ni halali na ambayo si halali. Maandamano ambayo si halali maanake yanaashilia uvunjifu wa amani ni maandamano ambayo yanaelekea kutenda uhalifu sasa kama ni maandamano yanakuja kwa njia ya uhalifu na jeshi la polisi lipo kwa ajili ya kuzuia uhalifu maanake ni lazima tuhakikishe maandamano hayo hayafanyiki hivyo ni lazima juhudi ifanyike kabla ya hayo maandamano kufanyika"
"Maandamano yakifanyika ambayo si halali uwezo wa kuudhibiti tunao sasa natoa ti salamu kwa wale ambao wanafikiri wataweza kufanya maandamano ambayo si halali ya kutaka kuleta vurugu ndani ya nchi ambao ni watu wachache wenye maanake ni lazima watapamba na jeshi la polisi ambalo linasimamia usalama wa nchi hii, lakini niwambie na wale vijana wadogo na wazazi, wazazi wajitahidi sana kulea watoto zao wajaribu kuwaambia watoto zao wasiingie kwenye kuvunja sheria kwani unaweza kuvunja sheria kirahisi ila madhara yake ni makubwa. Unaweza kuingia kwenye maandamano ambayo si ya halali halafu ukileta shida kubwa kwako na familia yako"
Mbali na hilo Kamanda Sirro alisema kuwa wananchi wengi ndani ya Tanzania wanataka kufanya maendeleo na hawapendi kabisa usumbufu na kusema watu ambao wanataka kuleta usumbufu wanacheza tu kwani watapamba naye.
"Wanacheza na hiyo mitandao sijui tumefika mia moja, mia mbili siju elfu moja wajaze wanachosema lakini nasema nafasi hiyo hawataipata" alisisitiza Sirro
Wewe siro madaraka ni dhamana usifikiri utakaa maisha hapo.fanya haki unauwa watu bila sababu ?mungu atakuhukumu wewe na wote mlausika na wanaokupa amri.Tanzania ni nchi tulivu lakini mnakoelekea mnataka kuiaribu.
ReplyDeleteKwenye maandamano mnapika risasi live .huu ni uuwaji na unyama .mungu kakuumbueni mmemuuwa mwanafunzi asie na hatia.na dunia inakucheneni anamani iliotengenezwa kwa miaka mnataka kuiondosha .Mungu ibarimai Tanzania na wabariki Watanzani. Ameen
AWAMU YA SITA IKIWA CHAMA KINGINE ATAKUWAJE HUYO?
ReplyDeletechama gani kwa mfano!!?? hahahaha WEMBE-NI-ULE-ULE dugu
Delete