Jaji Mkuu Aitaka Serikali Kuishirikisha Mahakama

Jaji Mkuu Aitaka Serikali Kuishirikisha Mahakama
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma ameishauri Serikali kuishirikisha Mahakama kwenye mipango yake ya uanzishaji wa maeneo mapya ya kiutawala ili kupunguza changamoto za upatikanaji wa haki kwa wananchi.


Akizungumza wakati wa ziara yake mjini Kigoma, Jaji Mkuu amesema mipango ya Serikali ya uanzishwaji wa Wilaya au Mikoa uzingatie pia uanzishwaji wa Mahakama na kwamba, Mikoa na Wilaya mpya ndizo zenye ukosefu wa Mahakama hali inayowafanya wananchi kufuata mbali huduma za Kimahakama.

Akitolea mfano wa Wilaya ya Uyui, Mkoani Tabora, Jaji Mkuu amesema, kutokana na Wilaya hiyo kuzunguka Mkoa, wananchi wake hulazimika kufuata huduma za Mahakama Kuu zilizopo umbali wa zaidi ya kilometa 377.

Amefafanua kwamba, kupitia Mpango wa Maboresho Mahakama itaanzisha Mahakama zinazotembea yaani Mobile Courts, kwenye maeneo yote yenye changamoto kama hizo kabla ya kujenga Mahakama kwa kuwa changamoto ya upatikanaji wa huduma za Kimahakama bado ni kubwa nchini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad