Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo.
Ameeleza kuwa hivi sasa vipo viashiria vinavyotishia usalama wa nchi, na kwamba hatua zinachukuliwa ili kudhibiti hali hiyo.
Jenerali Mabeyo amewaomba Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa
na Rais John Magufuli dhidi ya wizi, ufisadi na matumizi mabaya ya
ofisi za umma, kwa kuwataja hadharani watu wanaojihusisha na vitendo
hivyo.
Ametoa kauli hiyo jana wakati akifunga Maadhimisho ya Tamasha la
Mashujaa wa Vita ya Majimaji katika Viwanja vya Makumbusho ya Mashujaa
wa Vita ya Majimaji mjini Songea.
Mabeyo amesema vita dhidi ya wizi na ufisadi, iliyoanzishwa na Rais
Magufuli, si ya mtu mmoja, bali kila Mtanzania anapaswa kushiriki, kwani
mali zinazoibwa na baadhi ya Watanzania, zinapaswa kuwanufaisha watu
wote.
Mabeyo alisema badala ya kushughulika na uvunjifu wa amani, ipo haja
ya Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya
Tano, ambayo imedhamiria kuwatumikia wananchi kwa kuboresha huduma za
kijamii ili kutoa fursa kwa wananchi kutumia muda wao kufanya kazi za
kujiletea maendeleo.
Ametaja baadhi ya mambo yanayotishia usalama wa nchi kuwa ni matumizi
mabaya ya utandawazi ambayo mbali na ya kuharibu utamaduni wa nchi,
baadhi ya watu wanaitumia vibaya kwa kuhamasisha wananchi kufanya na
kushiriki katika matukio ambayo yanaashiria uvunjifu wa amani na utulivu
uliopo nchini kwa muda mrefu.
Jenerali Mabeyo alitaka shule za msingi, sekondari na vyuo nchini,
kufundisha wanafunzi umuhimu wa kulinda, kutunza amani na wananchi
kuishi kwa kupendana, badala ya kutumia muda wao kutafuta sababu za
kutengana, jambo ambalo halina tija kwa taifa.
Wakati huo huo, Jenerali Mabeyo aliitaka Wizara ya Maliasili na
Utalii kuboresha Makumbusho ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji ili yatumike
kwa ajili ya utalii na kuliingizia taifa fedha nyingi.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Chiristina Mndeme alisema Serikali ya
Mkoa wa Ruvuma, itaongeza nguvu katika kulinda mipaka yake ili wananchi
wa mkoa huo waweze kuendelea na kazi za uzalishaji mali.
Jenerali Mabeyo Ataja Baadhi ya Mambo Yanayotishia Usalama wa Nchi
2
February 28, 2018
Amesema vema kwani amani ya nchi inahusu kila mtanzania hata Kama hana chama
ReplyDeleteKWELI KABISA
ReplyDelete