Leo February 18, 2018 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia Askari Polisi sita kutokana na kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji NIT Akwilina Maftahmwenye miaka 22.
Mambosasa amesema February 16, 2018 CHADEMA walifanya mkutano wa kufunga kampeni katika viwanja vya Buibui Mwananyamala ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbowe alipanda jukwaani na kukatisha mkutano na kuhamasisha wafuasi wa chama hicho kuandamana.
SACP Mambosasa amesema kuwa Jeshi limeunda timu ya Upelelezi ili kuchunguza chanzo cha kifo cha binti huyo.
“Katika uchunguzi huo tunawashikilia askari 6 kufuatia tukio hilo pia silaha zao zinachunguzwa ikiwa ni pamoja ni pamoja na kuzipeleka kwa wataalamu wa milipuko,”-Kamanda Mambosasa
Pia Kamanda Mambosasa amesema Jeshi hilo linawachunguza watuhumiwa 40 ili kubaini kama miongoni mwao walikuwa na silaha za moto na linaendelea kuwatafuta wafuasi na Viongozi wa CHADEMA walioshiriki kushawishi wafuasi wao kushiriki katika maandamano.
Hapa polisi msilete visingizio.kazi zenu ni kuleta na kutunza amani. Tumewaona hadharani ni polisi ndio chanzo cha matatizo. Chadema walikuwa na sababu kuandamana. Wamelia kwa wiki nzima kudai haki zao makaratasi tu. Ni haki yao. Ni CCM na uongozi mzima wa Czczm wa kuulani kwa kunyanyasa wapinzani kwa muda wa miaka hii miwili. Sheria hazifuatwi na tume za uchaguzi. CCM mnapewa kila kitu na wapinzani mkiwanyima haki zao. Polisi mkishirikiana na CCM, tume ya uchaguzi hamfusti sheria za uchaguzi. Ni kutokana na hili Chadema imelazimila kudai vikaratasi tu kwa maandamano amayo ni haki ya kila chama kayika uchaguzi. Na ni mara ya kwanza namsikia Raisi wetu kudai na kufuatilia mauaji ya polisi hadharani. Ni mara ngapi polisi wamenyanyua risasi, piga wapinzani na amekaa kimya. Kukaa kwake kimya inamaana anakubaliana na uhalifu wa polisi zidi ya upinzani. Mawaziri eote kimya. Eti wanatimiza maagizo ya raisi. Mnawaona wapinzani wanavyouawa, nyanyaswa, na kudhararisjwa jadharani. Wengi na wabunge wenu mnaleta uchochezi kisa usjindi wa kichama ambao si ushindi wa Mtanzania.wako walalamikaji hewa bungeni kupitia CCM.akina Nape, mdukuma, na Bashe lakini ni unafiki mtupu. Ni kelele zisizo na tija. Inabidi wanaccm wote na maraisi watatu waliopita mko kimya mkijua wazi matatizo yote yanayotukabiri leo ni nyinyi mmeyasababisha. Eti mnayasawazidha leo lakini wote waliosababisha mko huru, mko madarakani na bado ufisadi mkuu unazidi kuendelea ndani ya ccm kila kukicha. Hakuna viongozi wenye milono misafi ndani ya chama chenu. Ndo maana mpo radhi kwa hsli na mali kubaki madarakani kwa nguvu kujipatia malupulupu makubwa.mnatumia mali za watanzania vibaya na kwa kupeana na kupendeleana. Mnalisafisha taifa, kulivua nguo linabaki uchi bila hadhi.
ReplyDeleteMpaka ifikie kama sAfrika kusini, Ethiopia, zimbabwe. Lakini Watanzania wengi mmekuwa waoga na kuzidi kuwakandamiza watu, kufuja mali, na mauaji ysmezidi nchini. Silaha ovyo ovyo, polisi wengine wakijihusisha, nchi hsina usalama sababu imebebwa na wahalifu wengi. Hiki kigo kisingetokea kama tume ingelazimishwa kisheria kutenda haki. Na msilaumu chadema. Mnawaonea. Walishalalamika mkaamua kukaa kimya ili washindwe uchaguzi. Polepole alisema mbele za watu lazima CCM ishinde kwa hali yoyote. Mayokeo ni vifo. Sasa mnawatafuta chadema. Kwa nini msiwaweke ndani tume ya uchaguzi.