Julius Mtatiro "Taifa Lilimpoteza Nyerere, Limemzika Kingunge

Taifa lilimpoteza Julius Nyerere, taifa limempoteza Kingunge! Kama unafuatilia historia ya taifa letu lazima utakuwa unajua kuwa ni mara chache sana taifa lolote linakuwa na wanasiasa wa haiba hiyo.

Taifa limekuwa na mamia na maelfu ya wanasiasa, lakini Nyerere na Kingunge ni EXCEPTIONAL! Na ukitafuta hao wanasiasa mahsusi na wa kipekee kwa sasa, ni kwa tochi!

Kingunge hakuwa mwanasiasa tu, alikuwa ni STRATEGIST wa hali ya juu. Nakumbuka siku niliyokutana naye ana kwa ana kwa mara ya kwanza nyumbani kwake, ilikuwa miaka 10 iliyopita.

Mimi na wenzangu tulikuwa kwake kumshawishi azungumze na Rais ili serikali ione haja ya kuongeza pesa za kujikimu za wanafunzi. Kikao kile kilikwenda jioni nzima na akakihamisha kesho yake asubuhi.

Mara ya pili kwenda kwake ilikuwa ni kuzungumza naye juu ya namna serikali ilivyokosea kutatua mgogoro baina yake na wanafunzi wa UDSM. Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga anaikumbuka ziara hii vizuri sana.

Mzee Kingunge anakusikiliza dakika 15 au ukipenda dakika 30, unazungumza wewe tu, ukimaliza, anaanza kupitia hoja zako zote na anazigeuzageuza anavyotaka.

Anakuonesha makosa ya serikali, anakueleza makosa ya wanafunzi, anakidadavulia uchuro wa uongozi wa chuo kisha anakwambia atakwenda kuzungumza jambo gani na Rais!

Leo hii hakuna BRAINS kama za Nyerere na Kingunge. Leo kuna hizi BRAINS zetu, za kawaida kabisa, za COPYING and PASTING, za kufoka na kutukana na kupiga risasi na kutisha na kuzuia na kutweza na kuumiza, kunyima dhamana na kufunga, kutafuta ukuu na kutafuta sifa.

Nitakuwa na fursa ya kueleza mengi kwa kina kuhusu ziara mbili ambazo nilishiriki na kuzungumza na mzee huyu muhimu kwa kirefu, nitafanya hivyo kwa njia maalum sana.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Mungu atusaidie tujenge hata robo tu ya uwezo aliokuwa nao Mzee wa taifa.

#Mtatiro J
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad