Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amkosoa Rais Kuhusu Katiba Mpya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amkosoa Rais Kuhusu Katiba Mpya
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amekosoa jaribio la Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kutaka kubadilisha Katiba ya nchi hiyo hatua ambayo itamruhusu kukaa madarakani kwa muongo mwingine au zaidi.


Katibu Mkuu Guterres amesema, upinzani na mashirika ya kiraia ni lazima yashirikishwe kwenye maamuzi yoyote ya kubadili Katiba ili kuzuia uwezekano wa nchi hiyo kutumbukia kwenye mzozo zaidi.

Ameongeza kuwa, anatambua Burundi kama nchi inayo mamlaka ya kujiamulia mambo yake kama taifa huru lakini akaonya kuwa jambo la kubadili Katiba linahitaji maridhiano ya pande zote.

Wakati huo huo muungano wa wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni nje ya nchi CNARED unaendelea kulaani jaribio lolote la kubadili Katiba, ukibaini kwamba hali hiyo utaitumbukiza Burundi katika machafuko, zaidi ya yale yaliyotokea tangu mwaka 1993 hadi 2004.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad