Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe baada ya Mbunge wa Mbeya mjini kuhukumiwa miezi mitano jela amesema kuwa ipo haja ya kufanya jambo ambalo dola itaamua kuwaweka jela wote na kutorudia walichofanya kwa mbunge huyo.
Zitto Kabwe amesema leo kuwa ameona mashtaka ya Mbunge huyo yaliyopelekea kuhukumiwa jela miezi mitano.
Wabunge wa Upinzani tusimame kuhesabiwa sasa,
Nimeona mashtaka ya Sugu yaliyopelekea kuhukumiwa kwenda jela miezi 5. Wabunge wote wa vyama vya Upinzani kwa namna moja ama nyengine tunasema haya kila wakati kwenye mikutano yetu. Kuna haja ya kufanya jambo ambalo dola itaamua kutusweka jela wote au kutorudia walichofanya kwa Sugu. Ninawasiliana na wenzangu tupate UNITED DEMOCRATIC FRONT,’ ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Facebook.
Hapa anachokizungumza Zito ni kitu gani? Hivyo Zito haelewi yakuwa sio raisi wa nchi tu bali hata raia wa kawaida ukimkutukana kama atachukua uamuzi wa kukupeleka mbele ya vyombo vya sheria unaweza kwenda jela. Vitendo alivyovifanya Sugu vya kumkashifu kiongozi wa nchi mbele ya wananchi vililenga kupelekea uvunjifu wa amani ulioweza kusababisha upotevu wa maisha na mali za watu kama si subira iliotukuka kutoka kwa wananchi wiokerwa na kauli za kishenzi za Sugu. Na kwa hekima ya wananchi baadala ya kumjibu pale pale waliamua kupeleka malalamiko yao kwenye vyombo husika na ni jambo zuri zaidi la sivyo wananchi wenye hasira wangeamua kumuadsbisha Sugu pale jukwaani we Zito unaeropokwa hovyo katika kutetea kila ovu inayofanyiwa serikali ungekuwa wa kwanza kusema wananchi wametumwa na serikali kufanya vurugu hizo. Ifike wakati tuwache siasa na kuviachia vyombo vya dola kutekeleza majukumu yake la sivyo tutaipeleka nchi yetu pabaya.
ReplyDeleteMheshimiwa unaendelea tu kupoteza mvuto wako kwa vijana kama wewe. Mimi ni katika waliokerwa sana na kauli ya Lissu alipoita waandishi kukufukuza chadema. Nahisi kumbe jamaa hawakufanya kosa. Ila inabidi ujiulize juu ya kauli zako.
ReplyDeleteUnazitoa kwa faida ya nani?
Je ungekuwa wewe madarakani ungeridhia mkuu wa nchi akashifiwe kadamnasi na bwa mdogo kama huyo kisa siasa?
Hiki si kipindi cha ujinga ujinga. Wanasiasa shindaneni katika kufanya mazuri mazuri kama mlivousiwa na Mkurugenzi wa zamani wa shirika moja maarufu hapo tz.
Hizo siasa za kipuuzi hazina tija kwa taifa wala wananchi wake.
Na kama kweli unadhani unachokihubiri umekikusudia, kwa nini basi usianze wewe upate kwenda jela?
Kwa nini unashawaishi wengine?
Fanya tukuone basi!