Kenya: Vituo viwili vya matangazo vya televisheni vyarejea hewani


Matangazo ya vituo viwili vya televesheni Kenya, KTN na NTV yamerejea hewani baada ya kufungiwa siku 7 na serikali.

Lakini bado haviwezi kutazamwa na Wakenya wengi ambao hawana king'amuzi.

Kupitia mtandao wao wa Twitter, NTV wamesema wamerudi hewani kwenye ving'amuzi vya "Dstv, GoTV and Zuku baada ya kufungiwa na serikali."

Stesheni ya iliyokuwa mmojawapo zilizoathirika na hatua ya serikali ,Citizen TV bado haijafunguliwa.

Serikali ilizifunga stesheni tatu za televisheni NTV, Citizen na KTN kwa madai kuwa vilipanga kupeperusha moja kwa moja matangazo sherehe ya kumuapisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kama rais licha ya onyo kutofanya hivyo.

Tutaendelea kuwaletea habari kadri zinavyotufikia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad