Kenyata Amtolea Uvivu Odinga Amtaka Aache Kumchafua

Kenyata Amtolea Uvivu Odinga Amtaka Aache Kumchafua
Ikiwa ni wiki moja imepita tangu Kiongozi wa Umoja wa Vyama vya Upinzani nchini Kenya kujiapisha kuwa Rais wa watu wa nchini hiyo, Hatimaye Rais wa Kenya anayetambulika kikatiba Uhuru Kenyatta amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu tukio hilo.

Rais Kenyatta amesema kuwa kujenga taifa ni kazi kubwa lakini kubomoa ni muda mfupi hivyo amemshauri Raila Odinga kuacha maneno yenye mizozo na kuchafuana nje ya nchi kwani kushindwa kwenye uchaguzi ni jambo la kawaida hata yeye alishawahi kushindwa na akajipanga tena.

“Kujenga ni ngumu lakini kupasua ni dakika moja, lakini hawaoni tabu kupasua afadhali apasue apate uongozi, awe mkubwa, ukubwa sio kiti ukubwa ukubwa ni vitendo ambavyo unawatendea wananchi ambao unataka kuwaongoza, na hivyo hivyo hata sisi tumekuwa twahimiza ni nini unawatendea wananchi wako. ukiwa umetoka nchi yako unaenda kutembea nchi nyingine kusema wale wanaoongoza kule wanastahili kufungwa. Si uje hapa Kenya kwetu utuambie,“amesema Uhuru Kenyatta huku akimshauri jambo la kufanya Raila Odinga.

“Huwezi kufanikiwa kwa kumtakia mwenzio mabaya, omba mwenyezi Mungu na uombe wananchi kwa njia tulivu uoneshe sera zako tofauti na sera za wale wengine na wananchi sio wajinga wapo na ujuzi wakuamua ni nani wanataka na nani hawataki. Kama hawakutaki safari hii we pumzika wacha wale wengine waendelee, mimi nimegombea mara nyingi, mimi nimewahi kusimama hii kiti nikashindwa na nikakaa nikatulia, Nikasema eehh Mwenyezi Mungu basi hii sio nafasi yangu wakati hii na nikakubali kushindwa, sasa ninaongoza na nitaongoza mpaka wananchi waseme basi wewe tulia, sasa shida iko wapi na tunabaki tunachafuana hapa kila siku, Lets us work together, Lets us keep Kenya moving ahead, lets us provide services to our people mambo hayo ndiyo ya muhimu na ndivyo tutaendelea na waseme na waseme hawatutishi,“amesema Rais Kenyatta kwenye kongamano la kuimarisha hali ya usalama nchini Kenya liliofanyika wikiendi iliyopita katika chuo cha Kenya School of Government (KSG) jijini Nairobi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad