Kiongozi wa Upinzani Aliyemuapisha Raila Udinga Ashtakiwa kwa Kosa la Uhaini

Kiongozi wa Upinzani Aliyemuapisha Raila Udinga Ashtakiwa kwa Kosa la Uhaini
Mmoja wa viongozi wa upinzani nchini Kenya Miguna Miguna ameshtakiwa na kosa la uhaini kufuatia kuhusika kwake katika kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Bwana Miguna alishtakiwa kwa kuhudhuria na kuidhinisha kiapo alichokula bwana Raila, kushiriki katika mkutano uliokuwa kinyume na sheria na kuhusika na maswala ya kihalifu.

Aliwasilishwa katika mahakama ya kaunti ya Kajiado yapata maili 50 kusini mwa Nairobi ambapo alitarajiwa kufika mahakamani.

''Kwa mara nyengine serikali inakiuka haki za bwana Miguna kwa kumsafirisha kutoka eneo moja hadi jingine bila ya kujulisha familia ama wakili wake'', alisema bwana Okero.

Baada ya kitendo ya kujiapisha, nini kinachofuatia kwa Raila Odinga?
Bwana Miguna angali katika mikono ya polisi huku akiwa hajulikani aliko licha ya kwamba mahakama ya Nairobi ilitaka aachiliwe kwa dhamana ya ksh. 50,000 siku ya Ijumaa.

Mnamo tarehe 30 mwezi Januari , bwana Miguna alikuwa kiungo muhimu katika kumuapisha Raila Odinga kuwa rais wa wananchi katika bustani ya Uhuru Park jijini Nairobi.

Siku chache baadaye, mnamo tarehe 2 Februari, alikamatwa katika uvamizi wa alfajiri katika nyumba yake baada ya kuwajaribu polisi kumkamata.

Viongozi wengine wawili wa upinzani pia walikamatwa.

Bwana Odinga na wafuasi wake walipinga matokeo ya uchaguzi wa mwaka uliopita ambao rais Uhuru Kenyatta alifanikiwa kushinda awamu ya pili katika uchaguzi wa marejeleo mwezi Oktoba.

Bwana Kenyatta alihifadhi kiti chake kwa kupata asilimia 98 ya kura mnamo tarehe 26 Oktoba ikiwa ni asilimia 39 ya kura zote zilizopigwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad