Kitwanga aikosoa Serikali ujenzi wa Reli


Mbunge wa Misungwi (CCM), Charles Kitwanga ameikosoa Serikali ya awamu ya tano na kuitaka iwe na mipango inayoeleweka na si kufanya maamuzi au mipango ya zimamoto.


Kitwanga amesema hayo bungeni na kudai kuwa Serikali haina haja ya kujenga reli nusu nusu ikiwa inaona haina mpango endelevu wenye tija na kuleta matumaini kwa wafanyabiashara na watu wa viwanda.


"Tunahangaika kutengeneza reli na reli inajengwa kutoka Dar es Salaam kuja Morogoro inawekwa reli ya umeme ila ukishafika Morogoro kuja Dodoma utofauti wa reli kati ya hiyo standard gauge na ya kawaida unatofautiana, sijui sasa unaanza kupakua hiyo mizigo uanze kupakua kwenye ile reli nyingine ya zamani? Mimi nadhani kuwe na mipango ambao unakuwa ni wa jumla utachukua muda lakini unajua tunajenga reli kutoka Dar es Salaam mpaka Kigoma au Dar es Salaam mpaka Mwanza" alisema Kitwanga


Kitwanga aliendelea kusema kuwa; "Lazima kuwa na mipango thabiti tunasema kwamba hicho ni kipindi cha mpito ambacho kitakuwa kinaeleweka kwa wafanyabiashara na watu wenye viwanda nchini ambapo watakuwa na matarajio yanaoeleweka na mipango hii ifuatwe 


"Hakuna sababu ya kuanza kujenga nusu nusu wakati hujui kinachofuatia na huna mpango wa kupata hela, ni vyema ukawa umejipanga kwamba nikitoka Dar es Salaam kufika Morogoro nitakuwa nimepata fedha kutoka Morogoro kwenda Dodoma, Tabora tusiwe na mipango ya zima moto" alisisitiza Kitwanga
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad