Kiwanda cha Dangote Chatoa Msaada ya Mifuko 2,400 ya Seruji Kwaajili ya Kuboresha Miundombinu ya Shule

Kiwanda cha Dangote Chatoa Msaada ya Mifuko 2,400 ya Seruji Kwaajili ya Kuboresha Miundombinu ya Shule
Wakati baadhi ya wanafunzi wa shule 10 za Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara wakisoma katika madarasa ya nyasi na chini ya miti,  kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo mjini hapa kimekabidhi mifuko 2,400 ya saruji kusaidia kuboresha miundombinu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa mkoa, Gelasius Byakanwa kufanya ziara katika halmashauri hiyo na kuzibaini shule hizo.

Ziara hiyo ilifanyika siku chache baada ya MCL Digital kuripoti wanafunzi wa Shule ya Msingi Mitambo kusomea chini ya miti ambapo kiliitishwa kikao cha wadau wa elimu na kutoa ahadi mbalimbali ukiwemo uongozi wa kiwanda hicho.

Akikabidhi saruji hiyo kwa halmashauri, Kaimu Katibu Tawala wa wilaya, Francis Mkuti amesema mkuu wa mkoa wa Mtwara aliitisha kikao cha wadau wa elimu na watu kuahidi vitu mbalimbali pamoja na nguvu kazi ili kuwaondolea wanafunzi adha wanayokumbana nayo na kuwawezesha kupata elimu bora.

“Nishukuru uongozi wa kiwanda cha Dangote, lengo la mkuu wa mkoa ni kuboresha miundombinu ili (wanafunzi) wapate elimu bora na kutuwezesha kutoka katika zile nafasi za mwisho na sisi tuweze kusogea juu, niwakumbushe wengine walioahidi na wao kutimiza ahadi ili kufikia azma tuliyokusudia,” alisema.

“Kila kitu tunafanya kwa hatua, naamini tukimaliza suala la madarasa itafuata miundombinu mingine ikiwemo nyumba za walimu.”

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri, Fundikira Masamalo amesema saruji hiyo itatumika kujenga madarasa 48 ya shule 10 zilizoonekana kuwa na hali mbaya.

Amesema halmashauri imeshaandaa vikundi vya vijana kwa ajili ya kufyatua matofali yatakayosambazwa katika maeneo yaliyoonekana kuwa na uhaba wa madarasa.

   
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad