Kocha wa Azam: Michuano Hii ni Migumu Hatutaki Kufanya Makosa

Kocha wa Azam: Michuano Hii ni Migumu Hatutaki Kufanya Makosa

Kocha wa Azam FC  Aristica Cioaba, amesema hataki timu yake ifanye makosa kwenye mchezo wa raundi ya 16 bora ya kombe la shirikisho nchini dhidi ya timu iliyopanda ligi kuu ya KMC.

Mchezo huo ambao unatarajiwa kupigwa jumamosi hii kwenye uwanja wa Azam Complex, Cioaba ameueleza kuwa ni mchezo muhimu kwa timu yake kutokana na timu hiyo kutaka kusonga mbele ya michuano hiyo.

“Hatutaki kufanya makosa na wachezaji wanafahamu michuano hii kuwa ni migumu kama huweki umakini wa kushinda mchezo basi utapata tatizo kwa kuwa ni mchezo mmoja tu na sio kama ligi'', amesema.

Azam FC inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ilitinga katika hatua hii baada ya kuifunga Shupavu ya Morogoro mabao 5-0. Wakati KMC  iliichapa Toto Africans ya Mwanza mabao 7-0.

KMC ni timu iliyopo chini ya Manispaa ya Kinondoni ya kuanzia msimu ujao itaanza kucheza ligi kuu baada ya kufanikiwa kupanda kutoka ligi daraja la kwanza.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad