Taarifa hizo ambazo zimetolewa na Shirika la Habari la Yonhap limeripoti kuwa Park, 66, alifukuzwa mwezi March, 2017 na ameshafunguliwa mashtaka juu ya tuhuma za rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na hata hivyo ameyakataa madai hayo.
Waendesha mashtaka hao pia wanataka Dola Bilioni 118.5 sawa na Tshs za Kitanzania Trilioni 283 kama faini kutoka kwa Park kutokana na makosa aliyoyafanya.
Mwanasheria anayemuwakilisha Rais huyo wa zamani Park Seung-gil, kwa niaba ya Park aliomba msamaha kwa kilio mbele ya Mahakama ya Wilaya ya Seoul akisema Park alijaribu sana kuongoza nchi mchana na usiku.