Korea kaskazini imezindua pombe mpya iliyotengenezwa kwa kutumia mbinu mpya na ya 'kipekee', inaarifiwa.
Kwa mujibu wa gazeti la serikali Rodong Sinmun, kiwanda cha kutengeneza pombe nchini Taedonggang kinadai kuwa mbinu yake mpya ya kutumia ngano badala ya mpunga ni bora zaidi kuliko pombe nyingine zilizoko kwa ladha na hata harufu nakwamba imepokewa vizuri na waraibu nchini.
Taedonggang kimekuwa kikitengeneza pombe tangu mwaka 2015, na hii huenda inatokana na shutuma kutoka kwa kiongozi mkuu nchini Kim Jong-un kwamba pombe inayoingizwa nchini kutoka Korea kusini haina ladha, jarida la kila siku huko Seoul Chosun Ilbo liliripoti wakati huo.
Kwa kawaida, vyombo vya habari Korea kaskazini vinaitangaza pombe hiyo kama ufanisi katika mpango wa Kim Jong-un kuinusha viwango vya maisha katika nchi hiyo ya kikomyunisti, vikisema ni kutokana na ' jitihada za muda wote"kuyafanya maisha "kuwa ya raha zaidi kwa raia".
Chosun Ilbo anadai kuwa Kim anapenda pombe , na anaeleza kuwa kwa wakatimmoja alijaribu kuidhinisha kampuni ya utengenezaji pombe PyongYang kama iliyopo katika nchi ya Ujerumani biergarten. Hatahivyo kwa mujibu wa taarifa kutoka Korea Times, kampuni hiyo ya Ujerumani ilikataa ombi hilo .
Lakini kutokana na mambo mengi yanayofanyika katika nchi hiyo, haijulikani iwapo taarifa hizo kuhusu biergarten ni za ukweli au ni uvumi tu.