Wote tunafanya kazi za kuajiriwa, hivyo tunatoka asubuhi tunarudi jioni, japo yeye anatangulia kurudi nyumbani. Sasa ana tabia ya kubeba kila umbea anaopata kutoka kwa mashosti zake na kuja kunisimulia mimi. Story za nani anatembea na nani, mke wa nani ana mahusiano na nani, mume wa nani anatembea na nani, nani ana tabia gani etc. Mimi huwa sina tabia ya kufuatilia maisha ya watu, nimejiwekea commitment kwa kazi yangu na familia yangu. Ya mtaani siyapi uzito, japo ni muhimu kujua ABC za kitaa.
Moja, Kuna jirani yetu ana duka, mke wangu akapata story kuwa yule mama na mumewe ni waathirika. Mwenzangu akatangaza marufuku kwenda kununua kitu chochote pale. Nikamweleza kuwa kama ukimwi ungekuwa unaambukizwa kwa style hiyo basi sijui kama kuna binadamu angebaki hapa duniani. Akaninunia.
Lingine linalofanana na hilo: Kuna siku alikuja akanisimulia habari za mama mwingine mwenye duka pale gengeni a.k.a. Mama J ambaye hana mume alivyo na tabia mbaya, Kuwa anawaingiza wanaume kwake anawabadilisha tu. Sikutaka kupoteza muda kwenye huo mjadala, kumbe yeye alitaka atoe ultimatum kuwa ni marufuku kwenda kununua bidhaa kwenye hilo duka. Siku moja akaniomba nimsindikize tukachukue maziwa mida ya jioni kwani mwenye kuuza hakuweza kuleta. Wakati huo, tulikuwa tunatafuta mayai ya kienyeji na upatikanaji wake ni wa shida.
Sasa tukiwa tunapita barabarani nikaona kwa duka la mama J ana mayai ya kienyeji tena mengi tuu. Saa ya kurudi nikashauri tuchukue mayai, akasema twende nyumbani. Nikamshawishi kwani upatikanaji wa mayai ni shida, tukapitia pale tukachukua mayai kumi. Pia nikanunua vocha ya tigo. Mama J akasema vocha iliyobaki ni ya kurusha. Nikamwambia poa nirushie, nikamtajia namba. Kumbe hapo ndo nikawa nimetibua nyongo bila kujua.
Tulipotoka pale njia nzima nikaona mtu kanuna hataki kuongea. Kufika home kaniita chumbani akaanza kunigombeza, eti mbona alishaniambia tabia za yule mama alafu bado naenda kununua vitu kwake?
Pili, nikipigiwa simu haijalishi ni muda gani na ni wapi, lazima aulize nani amekupigia na anasemaje. Ukweli hata nikimwambia hawezi kumfahamu kila mtu na siyo kila kitu naweza kumsimulia, mambo mengine ni ya kikazi. Kila wakati anapekua simu yangu kana kwamba niko polisi.
Tatu, tumebahatika kuwa na usafiri, na tunapokaa daladala ni za shida kidogo. Hivyo, kila asubuhi lazima tutoke wote, tumpitishe mtoto shule, then nimdrop yeye kazini. Sasa tukiwa njiani akimwona mtu yeyote anayemfahamu ananiamrisha tumpe lifti huyo mtu. Kumbuka mimi simwulizi kuwa huyo mtu ni nani wake. Nachukulia kawaida. Sasa ikitokea mimi nimemkuta mtu ninayemfahamu au rafiki yangu, huyo mtu akishuka kwenye gari, basi nitaulizwa maswali kama vile niko polisi nahojiwa. Na bahati mbaya ikiwa ni mwanamke, basi ananuna na wakati mwingine nikitaka kusimama anasema twende bana tunachelewa. Hii imenikera sana kuliko kawaida.
Sasa, kuna shosti zake wa karibu sana, mara nyingi nawapa lifti anapotoka kazini, basi anawasifia sana kuwa wana tabia nzuri, sometimes ananiomba tuwapeleke mpaka mjini japo sina ratiba ya kwenda huko. Sasa hao mashosti zake nimetembea nao na hajui. I just wanted to prove kuwa mambo yake ya kijinga hayanizuii kufanya nikiamua. Jamani kumlinda mpenzi ni sawa na kulinda samaki baharini, ukilinda Kigamboni wenzako wanavua bagamoyo.
Anyway, nipeni wazo mbadala nimfanyeje ili aelewe hilo somo?