Kutana na Mchezaji Ambae Ndani ya Misimu Miwili Mchezaji Amepandisha Timu Mbili Ligi Kuu

Songa Betheli ni mshambuliaji aliyeweka rekodi ya kupandisha ligi kuu timu mbili kwa misimu miwili tofauti, msimu uliopita aliisaidia Singida United kupanda daraja kitu ambacho amekifanya tena akiwa na Biashara United ya Musoma mkoani Mara.

Betheli ni miongoni mwa wachezaji walioisaidia singida kupada ligi kuu kwa kufungia magoli mengi timu hiyo lakini baada ya minziro kuondoka Singida United betheli aliondoka pia.

“Kwa sasa ni mchezaji wa Biashara United ambayo tumefanikiwa kuipandisha ligi kuu baada ya kazi ngumu lakini napenda kumshukuru Mungu kwa hilo. Nikilinganisha furaha niliyokuwanayo nikiwa Singida United ni tofauti na hapa Biashara kwa sababu nikiwa hapa nimeweza kuwa na mahusiano mazuri na wachezaji wenzangu, benchi la ufundi pamoja na uongozi mzima hiyo ndiyo tofauti na nilivyokuwa Singida United.”

“Nina uwezo ndio maana nakuwa kwenye timu na ninakuwa na mchango wa kufanikisha timu kupanda daraja, malengo yangu kwa sasa ni kucheza ligi kuu kwa kwa mafanikio kwa sababu umri haunisubiri.”

“Niliamua kutoka Singida United nikaenda Stand United lakini nikajiunga na Biashara katika dirisha dogo ili nije nijifue nifanye vizuri lakini pia nipate ‘title’, malengo yangu niliyojiwekea katika michezo mitano nikiwa Biashara nimeyatimiza, nimefunga magoli manne katika mechi tano nilizocheza, mchezo wa mwisho dhidi ya Transit Camp nimehusika katika magoli yote matatu tuliyofunga. Nimesababisha penati tukafunga goli la kwanza, nikafunga mwenyewe goli la pili nikatoa assist ya goli la tatu.”

“Mipango yangu ilikuwa kuja biashara kwa ajili ya kujifua lakini kwa sasa nitaipa kipaumbele Bishara kwa maana timu nitakayoichezea ligi kuu kama watakuwa tayari kukaa na mimi na kunipa mkataba.”

Songa anaungana na aliyekuwa kocha wake Singida United Fred Felix Minziro ambaye pia ameweka rekodi ya kupandisha ligi guu timu mbili tofauti katika misimu miwili mfululizo.

Mkoa wa Mara utashudia michezo ya ligi kuu Tanzania bara baada ya Biashara United kupanda ligi kuu kutokana na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya transit camp kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi C uliochezwa uwanja wa Karume mjini Musoma.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad