Le Mutuz: Historia ya Kweli Juu ya Maisha Yangu, My American Experience

Copy and Paste from lemutuz PART 1

safari yangu ya USA ulikua ni uamuzi wangu mgumu wa kuacha Ubaharia nikiwa Melini "MV. Luxemburg"ICMB Belgian Shipping Line tukiwa South China Sea tunatokea Shanghai/China tunarudi Singapore kazi yangu Melini nilikuwa Assistant Engineer au 0fisa wa Meli ndani ya Meli.

maisha ni kwa grade and class Maofisa mnaishi sehemu maalum na mnakula sehemu maalum na mna hang out sehemu maalum sheria za Meli hamtakiwi kuchanganyikana na Crew yaani Mabaharia wa kawaida infact hata Chakula ni tofauti Maofisa mnakula vizuri sana kuliko Mabaharia ...


l was a lucky man cause nilikuwa i ninasama Chuo Kikuu Cha Ubaharia Zeeman Marine Engineering College/Antwerpen, Belgium ambako nilijiunga nacho Miaka 4 na huu ulikua Mwaka wa Tano ninamalizia Leseni ya Uinjinia wa Meli ambayo ni Equivalent to Degree cause Melini zamani hakukuwa na Degree ila Leseni Only na Masomo ya Meli ni kila Miezi 6 Darasani na Miezi 6 unasafiri kufanya kazi Melini so by Mwaka wa Tano nilikuwa Baharia wa Ukweli nimetumia like 3 Years Baharini ambayo Practically katika Ubaharia inaitwa "SEA TIME" ambayo inaheshimika sana unapoamua kuomba kazi mpya ya Ubaharia Kampuni nyingine ndani ya Meli.


nilikuwa na Bosi wangu Engineer Feyerick Mzee aliyekuwa anavuta Cuban Cigar all the times binafsi nilikua sinywi Pombe wala kuvuta sigara hii ilinifanya kuwa Baharia maarufu sana ndani ya ile Melicause kila ljumaa tulikuwa tunapewa mgao wa Meli Katoni 5 za Beer, Katoni 2 za Sigara na Chupa 2 za Pombe Kali bure mimi nilikuwa always nabadilishana na Maofisa wengine wao wananipa Juice na Soda ...


Mzee Feyerick alikuwa na tabia ya kukaa chini na kunipa darasakuhusu Maisha nilikua kijana mdogo sana infact nilikuwa nimeichezea Miaka yangu kwenye makaratasi nikisaidiwa sana na Mwili Mkubwa lakini hata hivyo sura yangu ilikua inani betray always kuwa ni mdogo so nilikuwa natembea na Kitambulisho all the times ...

kama kawaida Mzee Feyerick my Bosi wa Engine Roomalinikumbusha sana kwamba Kijana mdogo achana na hii kazi ya Ubaharia haikufai i Nchi Kavu kasome utafute maisha bora ya kisasa", maneno mazito yalinigusa sana ..........ITAENDELEA PART 2..! From le Mutuz


Copy and Paste from lemutuz PART 2

my Boss Mbelgiji Feyerick alikua ananiambia the bitter truth kua niachane na mambo ya Meli akaniambia "Hii ni kazi ya Wazee na watu wasiokuwa na Maisha sio kwa kijana kama wewe" in all my childhood


nilikuwa naulilia Ubaharia nilianza nikiwa Jamhuri Primary School nilipokutana na "MABAHARIA WA NCHI KAVU" yaani Wanafunzi wenzangu Darasani kina Juma Jagan Burr (now in Canada) na Marehemu Raja Kaka hawa ndio Wanafunzi 2 walionipa the idea ya Ubaharia cause walikuwa na ndugu Mabaharia ambao walikuwa wakiwasaliana nao sana kutoka Nje l was in yaani "BAHARIA NCHI KAVU" Baba yangu mzazi then alikuwa Waziri wa Kilimo he was stunned kusikia kua nina mawazo ya kua Baharia alianza kusikia kutoka kwa marafiki zake ambao nilikuwa nawasumbua sana


kwa pembeni wanisaidie na ndato yangu nikimaliza tu Darasa la Saba they were all shocked that nitakuwaje Baharia at darasa la Saba tu? Baba yangu siku moja akanikalisha chini na akaniambia kuwa nisahau mambo ya Ubaharia its not for me settle kisaikolojia kuwa siwezi kuwa Baharia Darasa la Saba so nilichaguliwa kusoma Sekondari nikaendelea na masomo isipokuwa nikaanza Biashara ya kuuza Siagi


nikishirikiana na Rafiki yangu aliyenifundisha biashara hii Marehemu Koi Margai Mungu Amuweke Pema Peponi kila Jumamosi tunaruka na ndege ya Air Tanzania mpaka Musoma tunanunua siagi Kiwanda Cha Maziwa Musoma na kuirudisha Dar kuwauzia Wahindi tu hii mitaa ninayoshi sasa ndio maana ninawafahamu sana


mpaka leo kwenye kila safari tulikua tunapata faida ya at least Tsh, 20,000 wakati huo USD 1 ilikuwa Tsh, 10 tu nauli ya ndege kwenda Musoma na kurudi Dar ilikua Tsh, 950 tu Cargo tunalipia like Tsh. 3,000 kuileta Siagi kwa ndege na pia nikaingia biashara ya kuuza Dola za Kimarekani mtaani kwa bei ya ujanja.


officially nikawa a "MIDLLEMAN" mtu wa kati yaani mtu ukitaka kuuza anything hapa mjini ninakuuzia unanipa Kamisheni na Ninayemuuzia naye ananipa cha Juu Double kamisheni by the time namaliza High School nilikuwa na karibu Tsh. 1M Cash na USD 10,000 Cash Money nikaanza mipango ya kwenda Majuu ..ITAENDELEA PART 3 from lemutuz


opy and Pest from lemutuz PART 3

by the time nimefika Form Two I was a Super Street Smart nikaamua kuanza kuishi mwenyewe nikapata Studio Chumba kikubwa pale YMCA! pembeni ya Holidays In Hotel Downtown so nikahama kutokea lkulu kwa my Uncle Balozi Lusinde ambaye then alikuwa Waziri wa Mawasiliano


tulikuwa tunaishi nyumba ambayo sasa ni ofisi ya TAMWA tulikuwa kati kati ya Waziri wa Habari Marehemu Mwakawago na Waziri Mkuu Marehemu Kawawa na mabele yetu ni nyumba za Waziri wa Sheria Bomani na Waziri wa Fedha Jamal sijasahau mpaka leo the Good Life and the Bad life niliyoishi utotoni.

but all and all it was a good life after YMCA nilihamia Sido Hostel kati kati ya CBE na Maktaba ya Taifa hapa Kisutu Downtown so ni FACT that I have lived in Downtown almost all my life mpaka leo bado nipo Downtown


baada tu ya kumaliza Shule nikaenda JKT 0ljoro Arusha Mwaka mmoja kwa mujibu wa Sheria l was a Soccer Star na nilikuwa na Vijisenti so kila siku nilikuwa Dar naendelea na biashara zangu huku nipo JKT hahahaha nikirudi Camp nawapiga Chai Maafande no problem na nikicheza Soka timu ya Kikosi ninafunga magoli hakuna kelele za kwa nini sionekani Kambini...


wazo langu lilikuwa kwenda kutafuta Ubaharia lakini wa kusomea Shule 30 nika settle na idea ya kwenda Belgium Bongo enzi hizo ilikua huwezi kununua tiketi ya ndege kwa pesa za Tanzania mpaka uwe na kibali maalum kutoka kwa Gavana wa BOT wakati alikuwa Marehemu Nyirabu so nikaenda kuomba kumuona ofisini kwake kwa kisiingizo cha mtoto wa Waziri

nikaruhusiwa nukamuona lakini nikawa naomba Mungu asimpigie Baba yangu kumuuliza kama ameniruhusu so nilipokaa naye uso kwa uso nikaanza kumpiga porojo ili kumfanya asikumbuke a Baba yangu akaanza kucheka sana kufumba na kufumbua alishanipa Kibali cha kununua tiketi ya ndege kwa hela za Tanzania wakati huo USD 1ilikua Tsh. 16 na risiti ninazo mpaka leo

akaniambia niende kwa Mama Kimbe mama mzazi wa my Friend Matare Joseph Nyerere aliyekua 0fisa wa BOT ndiye aliyenimalizia paper work zote za kibali nikaenda Sabena Airways pale Samora Avenue ambapo sasa ni NHC Bulding nililipa Tsh. 120,000 nauli ya return to Brussels/ Dar itaendelea....PART 4!

PART 4: "MY AMERICAN EXPERIENCE"

Niliamua kuonana na Captain na kumfahamisha kua nimemua kuacha kazi ya Ubaharia for Good tukiwa njiani kutoka Shanghai/China to Singapore sheria za Meli ni Baharia akisema ameamua kushuka Meli hakuna mjadala so Captain akamfahamisha Agent wa Meli Nchi kavu aliyenipokea tulipofika tu na kunipeleka Five Star Furama Hotel ambapo nilipewa mapumziko ya siku 5 kabla ya kuruka na Singapore Airlines to Bombay niliko connect na Ethiopian Airlines to Bongo ambapo nilikaa miezi 2 na kuruka tena

...KWANINI NILIACHA UBAHARIA? baada ya kukaa Baharini niligundua kuwa maisha ya Baharini yalikuwa ni madogo sana honestly no life na sikujua kua Binadam ukikaa wiki nzima unaona maji tu bila nchi kavu akili zinacheza kidogo na all and all nikagundua Mabaharia wanaorudi Bongo walikuwa na mbwembwe nyingi ambazo ni uncalled and unfounded for as opposed na uhalisia na ugumu wa kazi na maisha ya Baharini waliyoyaishi ...sawa kulikuwa na pesa ambazo ukijinyima zinakuwa nyingi ila tatizo ni matumizi yake hasa baada ya kupewa hela nyingi kwa wakati mmoja so binafsi nina conclude my mission at Ubaharia as an adventure ya kupanuka Akili na Kusafiri almost Robo tatu ya Dunia ...

THE BERMUDA TRIANGLE ni safari za Meli kutoka Europe kwenda Brazili au Latin America ni sehemu ya baharini ya hatari sana that Kampuni ya Meli inakupa option ya kubadilisha Meli ili usiende na ukiamua kwenda unalipwa Mshahara mara 2 ya kawaida binafsi niliwahi kupita mara 3 huwezi kua a Real Seamen kama hujapita hapo na Meli ...

Ni kwamba Meli ikifika hapo tu inachukuliwa na Maji ambayo yanazunguka kwa kasi kubwa sana na kuifanya Meli kupoteza Control na kuishia kuwa Controlled na Maji sasa mnakuwa mnaelea tu na ni Maji yenye uamuzi mzunguke kwa siku ngapi kwa kawaida hua ni siku 3 mpaka 5 then one day Maji yanawaachia mnaondoka but kivumbi cha kuzungushwa bila kupenda ni balaa na hasa kwenye kulala mnapewa mito maalum na kuipanga pembeni na kulala kati kati kama kwenye jeneza siku 3 au 5 za kukosa usingizi ni hatari sana kwa binadam.... Brussels/Belgium one week nikaruka tena to Montreal/Canada to Ottawa nikachukua basi Greyhound to New York City/USA! ....ITAENDELEA!



PART 5: "MY AMERICAN EXPERIENCE"

Maisha yamenifundisha somo moja muhimu na chungu kwamba "MUNGU HAWEZI KUTUPA BINADAM AMBACHO HATUJAMUOMBA" yaani toka nikiwa mdogo nilikuwa namuomba Mungu just a "COMFORTABLE LIFE" kumbe sijawahi kumuomba niwe "SUPER BILIONEA" ndio maana sijawa cause kwa njia za safari ya maisha yangu nilimopitia nilitakiwa kuwa by now lakini simlaumu Mungu cause huenda kutokuwa kwangu na mapesa mengi ndio kumenisaidia kuendelea kuishi mpaka leo kwa raha na Amani ya ajabu so ninaendelea kumuomba Mungu aendelee kunipa a Comfortable life yaani maisha ya kula vizuri na kulala vizuri na pesa kidogo mfukoni na kufanya lolote ninalotaka ambalo lipo chini ya uwezo wangu kama kusafiri popote Duniani kwa ndege na kukaa Mahoteli mazuri ya kisasa I love that.

Niligundua siku nyingi sana toka nikiwa mdogo kwamba I was born different nilizaliwa Mwanaume tofauti sana Mama yangu mzazi na Mama yangu wa Kambo originally walikuwa ni marafiki wa damu walioishia kuzidiana Akili na kugeuka kuwa maadui wa Ajabu na mimi nikawa caught up in the middle ya Uadui wao na the worst is Mama yangu wa Kambo was very educated as opposed na Mama yangu Mzazi ingawa wote leo ni Marehemu lakini kivuli cha Vita yao ninapigana nacho mpaka leo na ndipo Mange anapoingia in my picture cause ni agent tu wa hicho kivuli cha Shetani anayenisumbua toka utotoni kutokana na Vita kali ya Urithi wa Mali za Baba yangu ni Vita ya ajabu na ya kitoto sana inayowahusisha watu wengi mpaka waliosoma lakini wamefunikwa na Chuki dhidi yangu ambayo ni purerly Foolish and unfounded just UNCALLED FOR ....

Mange alianza rasmi kunishambulia baada ya kurudi Bongo Miaka 6 iliyopita alianzia Facebook na mashambulizi ya yake ya kwanza aliongelea urithi wa Baba yangu kwamba nimerudi Bongo kutafuta urithi ninayo quote yake mpaka leo so I hope nimewasaidia wale mnaojiuliza sana Chuki ya Mange kwangu inatokea wapi? ni kwamba Mange anawawakilisha baadhi ya Maadui zangu wa Maisha ambao wangependa kusikia nimekufa kwa sababu wana wasi wasi kua nitawadhulumu urithi wa Baba yetu ambaye bado yupo hai na huenda hata tukaondoka sisi tukamuacha ....hahahahha....there I was ndani Basi Greyhound to New York City/USA...ITAENDELEA


PART 6:- "MY AMERICAN EXPERIENCE" ...

Ndani ya Basi la Greyhound kutoka Ottawa/Canada tunaelekea New York City/USA nilikuwa ninawaza nitakapofika New York City itakuwaje? Simjui mtu so sitakuwa na mahali pa kulala JE ITAKUWAJE? but nikajikumbusha jinsi nilivyokwenda Belgium mara ya kwanza Miaka 5 nyuma so ghafla tukafika Border kama kawaida ya Uhamiaji ya USA wakishaona Passport yako inaonyesha uliwahi kuingia USA na kutoka huwa hawana tatizo na wakati huu Rais wa USA alikuwa ni President Ronald Reagan baada ya kugongewa mhuri wa kuingia nikalala usingizi mpaka Saa Nne Usiku tulikuwa tayari tupo Port Authority, West Manhattan New York City/USA mtaa wa West 42ND Street ambapo ndio mwisho wa Mabasi yote ya Mikoani yanayoingia New York City....

Kuna Mbongo mshikaji wangu nilikuwa na namba yake ya simu aliahidi kuja kunipokea lakini dakika ya mwisho HAKUJA nikashuka na begi langu dogo la nguo kama kawa nikakuta Ma Homeless kibao wanajitayarisha kulala so nikatafuta mahali saafi nikatoa Blanketi langu cause ilikuwa ni Winter time January so kulala ni kwenye masofa ya Abiria wanaposubiria mabasi ya Usiku na Asubuhi so na mimi nikawa kama Abiria ninayesubiri Basi ilinichukua miezi 3 ya Beach life kama tunavyoita kwenye Ubaharia ...

Mwishoni tu mwa wiki ya kwanza nikawa nimepata kazi Dukani as a "STOCK PERSON" kwa Mshahara wa USD $ 5 kwa saa so kwa masaa 40 kwa Wiki nilikuwa ninalipwa USD $ 200 per Week so nikaamua kukusanya pesa kwanza kwa kuendelea kukaa bure pale Stendi ya Basi ...nikiwa kazini Dukani I was charming Kiingereza cha Kimarekani ni tofauti na cha Dunia nzima so to Americans I mean wateja wa Duka nilikuwa bonge la kichekesho na English yangu ya Europe sikuwa muoga kuongea huku nikiendelea kua kichekesho kwa Wateja hasa Wakina Mama pole pole nikaanza urafiki na Wasichana Wakizungu na Weusi cause Duka nililokuwa nafanya kazi lilikua linauza Vifaa vya Nyumbani sana ambavyo Wanawake ndio wateja wakubwa nikaishia kuwa rafiki na Mama mmoja Mzungu aliyeishia kunipeleka kwa mtoto wake aliyekua bosi wa Kiwanda cha Vifaa vya Umeme akanipatia kazi iliyoanza kunilipa USD 10 kwa Saa Moja ...ITAENDELEA!

PART 7: "MY AMERICAN EXPERIENCE"

Baada ya kuanza kazi ya mshahara wa Dola 10 kwa saa sasa nikawa napata Dola 400 kwa Wiki pia nikatafuta kazi ya Usiku kuanzia Saa Sita Usiku mpaka asubuhi Kituo cha Petrol mtaa wa Stanford Boulevard Mt. Vernon baadaye nikaacha nikawa nakaanga kuku KFC Usiku so kwa kazi zote mbili nilikuwa ninapata Dola 550 kwa Wiki ndio nikatafuta Studio ya Dola 100 kwa Wiki nikahamia kwangu sasa kwa mara ya kwanza after 3 Months za kuhangaika na pa kuishi in US maisha yanaenda fasta sana Unafanya kazi mahali Wiki moja then unahamia pengine hivyooo...

Now kazi nilizokuwa ninafanya hazikuhitaji Viza wala Papers cause zilikuwa ni kazi za Wafanya Biashara wanaokwepa kulipa Kodi guys haya mambo ya kukwepa Kodi hata Majuu yapo kwa hiyo walikuwa wananiajiri "Chini ya Meza" kule wanaita "UNDER THE TABLE" yaani unaajiriwa tu kishikaji shikaji ...nikaamua kutafuta kazi ya kunilipa vizuri kusudi nisome Shule always akili na mawazo yangu ndoto zangu zilikiwa ni EDUCATION kwanza cause nilifikiria sana kua nisiposoma nikiwa mdogo sitasoma tena na nilikuwa ninajua kua ndugu zangu wa Mama wa Kambo walikuwa wanasoma wakisukumwa sana na Mama yao aliyekua akitumia all influences za Nafasi ya kazi ya Baba yangu kuhakikisha wanasoma nilikuwa ninajiuliza nisiposoma nitakuwa mgeni wa nani one day? ..

Mungu alinipatia bahati kubwa sana in my life mpaka leo Sijawahi kunywa Pombe wala Kuvuta Sigara so pesa zangu zote nilikua naingiza Benki tu baada ya kulipia kodi ya Chumba cause now nilikua na uhakika wa Dola 2,000 kwa Mwezi Chumba Dola 400 zingine 600 mambo yote mengine na 1000 Benki but likaja tatizo la ID Card huwezi kuishi USA bila kuwa nayo nikajaribu kutafuta New York City ikawa taabu kidogo kuna rafiki yangu Baharia Alex alikuwa anaishi Boston/Massachusets State akaniambia niende kule ni rahisi kupata so nikaomba likizo ya Wiki kazini nikaenda Boston na kupata ID Card I was happy cause now kwa mara ya kwanza I was in the American System maana ID Card inaenda kwenye Databese ya System ya Taifa ..so nikarudi New York City nikaibadili na kuwa ya New York then nikaomba Social Security Card nikapata sasa nikaanza mbio za kusaka Leseni ya kuendesha Gari! ...ITAENDELEA!

PART 8: - "MY AMERICAN EXPERIENCE" ..

Baada ya kupata leseni ya Gari ya kawaida nikaamua kuanza kutafuta leseni kubwa ya kunifanya niendeshe Semi Trailers kazi ambayo ndio ilikua inalipa mshahara mzuri so nikaenda kufanya mtihani wake darasani nikashinda na kupata Kibali cha kuniruhusu kujifunza ili baadaye nikafanye mtihani wa Practical nikishinda niwe Dereva kamili so nikaenda kampuni ya American Harzardous Waste nikaomba kazi ya "UTINGO" ya kuwa msaidizi wa Dreva ili kusudi nipate nafasi ya kujifunza kuendesha nikafanye mtihani wa Leseni niwafanyie kazi Mzungu Jack Supervisor wa Madereva akaniajiri hapo hapo nikaanza rasmi kazi ya Utingo na kazi yangu ilikuwa kusafiri na Dreva na kumsaidia kushusha Makontena ya Harzadous Waste kwa kutumia Hydraulic Lift ambayo imefungwa nyuma ya Truck nilipewa Mzee wa Kijamaica kwa Jina Errol aliyeishia kunisaidia sana kuelekea kupata leseni yangu ...

Now tulikua tunaanza kazi Saa Moja Asubuhi tunatokea Yard The Bronx Market Terminal nyuma ya The Yankee Stadium Bronx tunaingia Manahattan au Brooklyn inategemea kila siku route zilikuwa zinabadilika na kazi yetu ilikuwa ni service kwa Hospitali Kubwa na Ndogo zote it was a fun Job kwanza ilikuwa inanipa nafasi ya kuijua New York City na Vitongoji vyake na pili ilikuwa ni kazi yenye Overtime sana kwani ni almost impossible kuifanya kwa masaa 8 tu kama inavyotakiwa so sasa nikawa na uhakika wa Dola 600 kwa wiki na bado pia nilianza kazi mpya ya kusafisha Jumba la Cinema Co-op City/Bronx ni kazi ambayo nilikua naingia Saa Sita Usiku mpaka Asubuhi ..

Kazi yangu usiku ilikua kusubiri Cinema iishe kuonyeshwa like Saa Sita na Nusu au Saba ninapewa Ukumbi wangu mkubwa mmoja kuusafisha mpaka Asubuhi I was fast nilikua na uwezo wa kusafisha kwa Masaa 2 tu ni kazi ambayo ilikua na changamoto moja kubwa kuondoa Big Gee kwenye Kapeti lakini tulikua tunapewa Special Spray inaondoa mara moja the best of this job was chenji wanazoangusha Watazamaji wa Cinema wakiwa kwenye viti ambavyo vinakua vimepinda ni kazi ambayo nilikua naifanya kwa siku 7 na nilikua na uhakika wa kuokota angalau Dola 10 to 20 kila siku ambazo zilikua nyingi sana kwa maisha yangu madogo sana....ITAENDELEA!

PART 9:- "MY AMERICAN EXPERIENCE"

Now nilikua napiga kazi ya kusafisha usiku fasta in 2 hours ukumbi una AC na Kapeti saafi so namaliza kazi like Saa Tisa natafuta kona moja safi nalala mpaka Saa 10 na Nusu naamka naingia kazini kwenye Trucks kule nako nilijiwekea tabia ya kuwahi mapema kusudi nipate nafasi ya kujifunza kuendesha mwenyewe na nilianza na kujifunza kurudi nyuma kwa muda mrefu by the time saa ya kuanza kazi ikifika nilikua nimeshatumia like lisaa limoja na mazoezi.

Baada ya Mwezi mmoja nikawa na uwezo wa kuanza kuendesha ila masharti ya Permit ni lazima niendeshe nikiwa na Dreva mwenye leseni kamili kwa sasa kazi zangu zote mbili zilikua zinanilipa Dola 1000 kwa Wiki kama kawaida naziweka Benki tu cause lengo langu lilikua kusoma tu! ...

Nilikua ninafanya kazi kama Punda mpaka sifa zangu zikaanza kuwafikia Wazungu na hasa mwenye Kampuni Msichana Mdogo Dina Muamerika Mtaliano aliyeachiwa Urithi na Baba yake na Mumewe Russ so siku moja Supervisor wangu Jack akaniita na kunipa Great News kua mwenye Kampuni ameniruhusu kuanza kufanya kazi peke yangu yaani nitakua ninaendesha Truck lenye Mataili 18 peke yangu yaani nitakua ninavunja Sheria kwa kuendesha na Permit tu Mzungu Jack akaniambia kuwa makini sana isipokua ukikamatwa tu akanipa namba maalum ya simu ya kupiga Mungu mkubwa sana .

Niliendesha kwa miezi 6 bila kukamatwa na sasa ndio umaarufu wangu wa kupiga kazi Fasta na Perfectly na Consistency ukaanza kua ndio the talk of all my Co-workers mpaka Viongozi wangu wa kazi ...lakini kwa mara ya kwanza in my life nikaanza kugundua kua KUMBE NINA UWEZO MKUBWA WA KUFIKIRI cause Wazungu ndio walioanza kunijadili sana nikiwa sipo na nikawa ninapata feed back kutoka kwa wafanyakazi wenzangu ambao hawakuwa wanapendezwa na sifa zangu za kupiga kazi.

Baada ya Miezi 6 sasa nikawa tayari kwenda kufanya mtihani wa Leseni CDL CLASS A & HAZARDOUS MATERIALS ni Leseni kubwa sana USA ni wachache sana wanazo maana ukishaipata unakuwa a Professional Driver unaweza kusafirisha mpaka Uranium au Silaha kitu ambacho the American Authority wanakiogopa sana sikulala usingizi siku ya kwenda kufanya mtihani sikua naamini kwamba hatimaye nitaipata hiyo Leseni...ITAENDELEA!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad