Mahakama Yamuhukumu Miezi 16 Jela Sanchez

Mahakama Yamuhukumu Miezi 16 Jela Sanchez
February 9, 2018 nakusogezea stori kutoka kwa Staa mpya wa klabu  ya Manchester United Alexis Sanchez amehukumiwa jela miezi 16 kutokana na kosa la kukwepa kulipa kodi.

Hukumu hiyo imetolewa February 8, 2018 , Sanchez anadaiwa kukwepa kulipa kodi wakati alipokuwa nchini Uhispania ambapo mamlaka nchini humo zinasema anadaiwa kiasi cha pauni laki tisa.

Kwa mujibu wa sheria za Hispania, hukumu ya kosa hilo haizidi miaka miwili jela, lakini badala yake amelipa pauni 525,000 kutokana na kosa ambalo alilifanya miaka mitatu alipokuwa akichezea klabu ya Barcelona.

Hukumu ya Sanchez imekuja katika kipindi ambacho bado mamlaka za mapato nchini Hispania zinafanya uchunguzi kuhusu kocha Jose Mourinho anaye tajwa kufanya kosa kama hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad