Dkt. William Morris aliwasilisha maombi mahakamani hapo akiomba mkewe, Mwingira na mtoto wake (9) wafanyiwe kipimo cha kujua vinasaba vya mtoto (DNA).
Dkt. Morris ambaye ni mume wa (mdaiwa wa pili, Phills Nyimbi) aliiomba mahakama itoe amri ya mkewe, Mwingira na mtoto wakafanyiwe kipimo hicho cha DNA ili aweze kujua wazazi halisi wa mtoto aliyezaa na mkewe.
Alidai mchungaji Mwingira alizini na mkewe na hatimaye kuzaa naye mtoto wa huyo wa kiume.
Akisoma hukumu hiyo leo Februari 26, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, amesema Dkt. Morris katika kesi hiyo ameshindwa kuonyesha mahusiano ya kimapenzi kati ya Phills na Mchungaji Mwingira.
Pia ameshindwa kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa na mke wa Morris ni matokeo ya mahusiano ya kimapenzi kati ya Phills na Mchungaji Mwingira.
Hivyo mahakama imeitupilia mbali kesi hiyo na kusema mdai ameshindwa kuthibitisha madai yake katika kiwango kinachotakiwa katika mashauri ya madai na alipe gharama.
Desemba 28, 2011, Morris na Phills walifunga ndoa ya kanisani na wakati wa mahusiano yao, Phills na Mchungaji Mwingira wanadaiwa kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na kupata mtoto wa kiume.