Mahakama YawatiaHhatiani Sugu, Masonga

Mahakama YawatiaHhatiani Sugu, Masonga
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imewatia hatia mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite aliyeanza kusoma hukumu leo Februari 26,2018 saa 03:32 asubuhi amesema washtakiwa wana hatia kwa makosa waliyoshtakiwa.

Baada ya kuwatia hatiani washtakiwa, hakimu Mteite anasubiriwa kutamka adhabu dhidi yao.

Sugu na Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni uonevu tu hakuna haki tabzania .mahakama polisi wote ni waonevu.
    Tuna toka wapi na tunapelekwa wapi ?
    Baba wa Taifa alisema .nanukuu, akuna nchi iliyokuwa salama katika hii dunia. Tizama Somalia 99 wanazungumza kugha moja dini moja .mfano mdovo huo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa hiyo ulitaka watu watukane tu eti? na wakishatukana waachwe? kwani hawawezi endesha siasa bila kutusi wengine? Acha kauli za jumlajumla, eti hakuna haki Tanzania, isingekuwepo hiyo haki unadhani hata kuandika ulichoandika ungeweza?

      Delete
  2. Watu wengine wamezoea kulalamika tuuu...kwan sheria katengenezewa raia na so mwanasiasa?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad