Majeruhi wa Risasi Maandamano ya Chadema Wapata Dhamana

Majeruhi wa Risasi Maandamano ya Chadema Wapata DhamanaLeo February 28, 2018 Watu watatu wanaodaiwa kuwa wafuasi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na shtaka la kufanya mkusanyiko isivyo halali.

Hata hivyo, watu hao watatu wameunganishwa katika kesi ya wafuasi 28 wa CHADEMA ambao walifikishwa mahakamani hapo wiki iliyipita.

Washtakiwa hao watatu walisomewa kosa lao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita.

Wakili Mwita aliwataja washtakiwa hao watatu kuwa ni Isack Ng’aga, Erick John na Aida Olomi.

Wakili Mwita amedai washtakiwa hao, March 8, 2018 wataunganishwa na wenzao 28, ambao walifikishwa mahakamani hapo wiki iliyopita.

Kwa pamoja wanadaiwa kuwa  February 16, 2018 huko Kinondoni katika eneo la Mkwajuni lililopo katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, walifanya mkusanyiko usio wa Halali kinyume cha sheria.

Inadaiwa kuwa mkusanyiko huo ulikuwa na nia ya kufanya uvunjifu wa amani na kusababisha Taharuki kwa wananchi.

Washtakiwa wote walikana shtaka hilo na wapo nje kwa dhamana kwa kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja ambaye alisaini ahadi ya Shilingi Milioni 1. 5 na wasitoke nje ya jiji la Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama. Upelelezi bado haujakamilika. Kesi imeahirishwa hadi March 8,2018.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hovyoo! Yaani unakubali kuandamana kijinga sababu ya uchaguzi!!! Huyo unayemuandamania hata akujui, na hata akipata akutambui.....hivi nyie watu wa chadema mtazinduka lini kuachane na huo ujinga wa kufuata mkumbo?? Hamkumbuki yalowapata wenzenu waloandamana Arusha???? Haya, umeshavunjwa mguu, huyo Salum Mwalimu na kundi lake wataku hudumia au mzigo umeupeleka kwa wazazi na nduguzo? mfyuuuuuuuu siku nyingine UTAKOMA AU UTAZIDI chaguo ni lako

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad