Assalam aleykum waungwana,
Mimi ni Muislamu mwenye akili timamu na ninaitakidi Sheikh ni Muislamu mwenzangu.
Huwenda baadhi ya watu watahisi kama mimi sio Muislamu ila nimetumia mwanya huu kukashifu hii dini lakini hapana jamani mimi ni Muislamu japo sio maarufu hata mtaani kwangu, lakini hilo halinizuii kusema au kujadili.
Maneno ya sheikh kwa huyu dada Mange Kimambi kama ambavyo wengi wetu tumesikia sioya sawa kabisa hasa kitendo cha yeye kusema huu ndo mwaka wa mwisho kabisa hatotukana tena sasa mwaka wa mwisho kivipi?
Haoni kama kajiingiza kwenye dhana mbaya na watu wahisi kama atafanya watu wamhisi vibaya au wahisi kama Uislamu kweli ni uchawi wa kutupiana majini na mashetani?
Kitendo chake cha kukata kwa kusema huu ndo mwaka wa mwisho na kama keshajua kitakachomtokea huyo binti kwa huu mwaka na huko tunasema ni kujua ghaibu(mambo yaliyofichikana ya baadae au sasa)na hilo jambo liko kwake Allah na sio kwa kiumbe yeyote yule.
Nafasi yake kama kiongozi wa dini alitakiwa atumie nafasi hiyo kumfahamisha Mange kwa maneno mazuri kabisa huwenda angefahamu huyo Mange kwa sababu yeye shekhe hakuwekwa kuhukumu bali kawekwa kuwaelimisha watu na sio vinginevyo na hatakiwi kushindwa walakukata tamaa juu ya mtu fulani.
Huyo Mange ni mara ya ngapi hii kuwatukana sheikh Alhadi? Si ndio ya kwanza tu? Vipi sheikhe Swabru (subira)iko wapi?
Kusema hivi simtakasi na wala hakutomtakasa Mange Kimambi laa bali tunafahamu kwamba anachofanya sio sawa lakini sisi tumeona shekhe wetu anasikika na kasimama kwa niaba ya waislamu sasa huwenda watu wakaona kama uislamu umeruhusu au ndivyo uislamu ulivyo mtu akikuvunjia adabu basi utoe kitisho au ukamshitakie kwa Allah kwa lengo la kumzimisha na sio kwa lengo la kubadili uovu wake uwe mwema.
Hata mtume wetu enzi hizo alikuja muarabu wa mashambani(bedui)akakojoa msikitini watu wakahamaki wakataka kumpiga lakini bwana mtume akawakataza na akamuita yule bedui akaanza kumpa maneno malaini kana kwamba kapatia kile kitendo kumbe ni kosa kubwa sana.
Ikiwa huyu kanajisi nyumba ya ibada mbele ya mtume wa Mungu lakini kapewa maneno malaini na hakupewa vitisho, vipi aje mtu amtukane mtu tena kwa sababu za kidunia tu ukaanze vitisho na mashtaka?
Shekhe anatakiwa amuombee kwa Mungu dada huyo aache tabia hiyo na azungumze kwa mema kabisa kwenye mitandao hiyo ja kijamii.
Wengine watanilaumu watasema mara ooh kama nasaha si ukampe kwa siri mbona unatoa hadharani.
Nasema hivi"""nasaha za siri ni kwa yale makosa ya siri mfano mtu kazini kwa kujificha au kaiba basi hapo unatakikana ukamnasihai kwa siri kwa sababu lile jambo halikuenea kwa watu lakini akifanya jambo hadharani kabisa na watu wakalichukulia ni sawa basi hapo lazima utoe nasaha au umkosoe hadharani ili kuwaokoa hawa watu walioamini jambo hilo.
Hivyo kauli hiyo yenye kitisho haikuwa sawa kabisa kabisa.
By Lelelu/JF
We hapo juu si muislam bali ni mnafiki mkubwa. Unatetea maovu halafu unajiita muislam .Huyo mange Kimambi hana mkubwa hana mdogo yeye kazi yake kukashifu watu tu. Sheikh hakuzungumza uchawi wala nini. Alichokisema sheikh Mange Kimambi anadhulumu nafsi za watu kwa kuwavunjia heshima bila sababu. Na kama vile haitoshi Mange Kimambi anatukana viongozi wa dini sasa mchana kweupe.Sheikh alichokisema ili kumrudi Mange Kimambi na tabia yake chafu wameamua kupeleka mashitaka yao katika Mahakama ya mbinguni. Hakuna jaji wa haki isipokuwa M/Mungu peke yake. Sasa mnaanza kuharahara hovyo hata mambo bado suburini haki itendeke. Yeye Kimambi kama bado akili angali nazo ni vyema kuomba radhi la kama anataka kusubiri kuona itakuwaje basi muache aendelee kutukana tu.
ReplyDeleteWeee, unasema ndio mara yake ya kwanza kumtukana shekhe, unataka awatukane mara ngapi??
ReplyDeleteHebu jifanye kama huyo shekhe alotukanwa ni baba yako, ungejisikiaje?? Khaa, hebu mwacheni huyo mange kimavi limpate la kumpata, kayataka mwenyewe kwa kukosa adabu kwake......mfyuuuu ASO-FUNZWA-NA-MAMAYE-HUFUNZWA-NA-ULIMWENGU