Marekani Yatoa Neno Kuhusu Mauaji Yanaoendelea kwa Viongozi wa Chadema

Marekani Yatoa Neno Kuhusu Mauaji Yanaoendelea kwa Viongozi wa Chadema
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umeweka wazi kusikitishwa na taarifa za kutekwa na utumiaji nguvu kikatili uliosababisha kifo cha Katibu wa CHADEMA kata ya Hananasifu Daniel John.


Taarifa hiyo kutoka ubalozi wa Marekani kwa vyombo vya habari  imesema kwamba tukio hilo la mauaji la makabiliano ya kihasama na vitendo vya kikatili ni jambo linalotia wasiwasi na kusikitisha sana.

‘’Tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia na marafiki wa marehemu kwa msiba huu. Tunatoa wito kwa vyama vyote kulinda amani na usalama wa mchakato wa kidemokrasia, taifa na wa watu wa Tanzania’ ’imesema taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo imeongeza kwamba  ‘’Tunaungana na Watanzania katika kutoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wenye uwazi ili kuwawajibisha wale wote wanaohusika na vitendo hivi vya kikatili kwa mujibu wa sheria za Tanzania".

Kiongozi wa CHADEMA kata ya Hananasif Kinondoni, Daniel John ameuawa kwa kukatwa mapanga baada ya kuamriwa kuingia kwenye gari na baadaye mwili wake kuokotwa kwenye ufukwe wa ,Coco Beach' ukiwa umekatwa mapanga sehemu mbalimbali.

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mauaji ni vitendo vya kihalifu hutokea popote pale duniani. Na zaidi ni masuala ya ndani ya nchi husika ila kuna wapumbavu fulani wa kitanzania wanaona fahari nchi yetu kuingiliwa uhuru wetu wa ndani na mataifa ya kigeni.

    ReplyDelete
  2. Ninawasiwasi na wachina nchini mwetu. Kila mtanzania inambidi awe macho nao.wameingizwa nchini, wakitoa vimisaada hapa na pale hasa Dar kwa mkuu wa mkoa. Mchina kwa sisi tunayemfshamu hana ubinadami. Na dhana za kivita, mabom i, washawadha vingi vinatoka huko. Mchina mshenzi anapokuwa mtafutaji. Ataiba kwa nguvu, atapora, na atatumia silaha youote pia kuua. Mchina pia ataingiza madudu ya hovyo, kemikali. Baruyi, cjakula ambacho si chakuliwa na binadamu. Ukimwacha mchina na wavhina wenzake wakamiliki sehemu mmekwisha. Kutoksna na uwimgi wao uchina Afrika ni mbinguni.watafanya shamba la bibi, na kuisafisha nchi. Mchina asikubaliwe kuanzisha kampuni binafsi bila kwenda na ubia na mtanzania. Atawachekea vizuri atawaua , ataharibu mazingira ya ncina atawaleta watumwa nvhini wafanyie kazi bure kama watumwa. Na atafanya kila kambo kuingilis madaraka ya nchi.na huenda wamejipenyeza pengi tu.
    Kwa msimu ujao tunamhitaji raisi na viongozi wenye maono na di wababaikaji kwa kulinda maslahi ya nchi na watanzania. Na mikataba yote na mchina ichunguzwe.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad