Maskini!.... Shida Zamfanya Mama Akamue Maziwa Yake na Kuuza Mtaani

Nimeipata hii stori ambayo inaweza kukuacha mdomo wazi mtu wangu ni kumhusu Mwanamke mmoja anayenyonyesha, ameshangaza watu siku za hivi karibuni baada ya kutangaza kuuza maziwa yake anayonyonyesha ili apate pesa ya matibabu ya mwanaye ambaye yuko mahututi hospitali nchini China.

Mwanamke huyo na mumewe walitengeneza video ya kutoa tangazo hilo, video hiyo ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii nchini humo na kuamsha hisia tofauti za jambo hilo kwa watu mbalimbali.

Mtoto huyo ambaye yuko katika chumba cha wagonjwa mahututi anahitaji Dola 1600 sawa na Tsh Mil 3.8 ili matibabu yake kufanikiwa. Mwananmke huyo na mumewe wanaripoti kukaa mtaani mume akishikilia bango la biashara hiyo huku mwanamke akikamua maziwa hayo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad