Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Mhe Lazaro Nyalandu amejikuta akipata wakati mgumu kuuaminisha umma kuwa jina linalotumika mitandaoni kutangaza safari ya kwenda Israel sio lake, hii ni baada ya Watanzania wengi kuomba nafasi baada ya tangazo la kwenda kuzuru nchini huko kutangazwa mtandaoni
Mhe Nyalandu amesema kuwa akaunti hiyo ya Facebook ambayo inatumia jina lake, sio yake hivyo watu wote waliojaza fomu na kumpatia namba mtu huyo wasiendelee kufanya hivyo kwani ni tapeli wa mitandaoni.
“Fake News alert❗Habari hii ya kupeleka watu Israel sio ya kweli na Account iliyotumika kuandika sio yangu. Tafadhali ipuuzeni. So many sad people out there wanaokaa kutungia wenzao UONGO. Sad!,”ameandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kuutarifu umma na kuweka tangazo hilo.
Tayari zaidi ya watu 400 wameshaomba kwenda kuzuru nchini Israeli baada ya tangazo hilo kuwekwa na mtu huyo anayejiita Lazaro Nyalandu.