Mbowe ' Usalama wa Taifa Wanaratibu Mikakati ya Kuwabambikizia Kesi wana CHADEMA'


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kimeongea na waandishi wa habari leo katika Makao makuu yao

Mbowe amesema Usalama wa Taifa wanaratibu mikakati ya kuwabambikizia kesi wana CHADEMA na wao wamejipanga kutokana na huo mkakati. Amemwambia Rais Magufuli kuwa wapo tayari kwa lolote maana wanapigania demokrasia

Mbowe amesema Mkoa wa Morogoro unaongoza kwa kuwabambikizia kesi viongozi wao. Lakini hata kwa mauaji, Mkoa huo unaongoza maana kuna historia ya watu wa CHADEMA kuuawa.

Amemuhusisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Amosi Makala kwenye kuratibu kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi(Sugu).Amesema hukumu ilifahamika na ilipangwa Hotelini, wote walifahamu na Amosi Makala anajua hilo

Aliongeza kwa kusema “CCM kama wanataka kurudisha uhalali wao wa uongozi waseme na wananchi watawaelewa na sio kutumia bunduki kukatisha uhai wa watu. Halafu tumeshaanza kuzoea kuuwawa, hili jambo si zuri maana tunakoelekea ni kutaka kuua upinzani”
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mbowe unatapatapa na kuhangaika bure kama mfa maji anyejaribu kuyapigia kelele maji na kuyakamata wakati ukijua dhahiri maji hayawezi kukisikia wala hayawezi kukamatika utazama tu. Malalamiko gani ya kudai CCM inataka kuua upinzani? Upinzani gani wa kisiasa uliokuwa nao CCM Tanzania hivi sasa? Mbona huo upinzani unaodaiwa kutaka kuuliwa ulishakufa zaamani tu na kilichokibakia ni vurugu za kisiasa kutoka kwa wanaojiita upinzani. Mbowe kama umeamua kuhamasisha wafuasi wako kutotii sheria za nchi kuna watu wapo tayari waliokuwa trained kwa mapambano zidi ya wanaotaka kuvunja sheria za nchi na hahilisi mtu wa chama gani . Upinzani wa siasa Tanzania umekufa na sasa Mbowe anaendesha genge la wahuni kujaribu kuwachanganya wananchi na kuleta machafuko Tanzania . Nia ya Mbowe na genge lake la kihuni ni kuwatoa watanzania na serikali yao katika focus kwenye vita zidi ya maendeleo . Wakati mwengine unaweza kuilaumu serikali kwa kuwachekea chekea na kuwalealea hawa akina Mbowe mpaka wanapata Jeuri ya kuthubutu kutamka hadharani kuwa wapo tayari kuanzisha vita vya ndani na serikali. Kiongozi wa siasa na genge lake mwenye malengo ya kuanzisha sivil war vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini badala ya kuhubiri amani wa kazi gani? Ndio pale tunaposema hakuna cha demokrasia wala nini hawa watu lengo lao ni kuleta vurugu nchini kwa hivyo inapotokea kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria lazima waadhabiwe adhabu kali za mfano sio kufungwa miezi mitatu au minne jela kamwe hawawezi kujifunza.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad