Mchezaji zamani wa club za Man United, Celtic na timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland Liam Miller amefariki dunia leo baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa kwa miezi kadhaa sasa.
Liam Miller amefariki kwa kusumbuliwa na kansa ya kongosho na aligundulika kuwa na tatizo hilo toka mwezi November mwaka jana na kuanza kupatiwa matibabu nchini kwao Ireland na United State, Liam hadi umauti unamfika alikuwa na umri wa miaka 36.
Kiungo Liam Miller akiwa na club ya Celtic 2003/2004 aliichezea michezo 44 na kuisaidia kutwaa Ubingwa wa Ligi msimu huo, mwaka 2004 Liam alijiunga na Man United na kudumu nayo kwa miaka miwili hadi 2006 alipoamua kujiunga na Leeds United kwa mkopo na baadae Sunderland.