Meya wa Iringa Apandishwa Kizimbani kwa Kosa la Kutishia Kuua

Meya wa Iringa Apandishwa Kizimbani kwa Kosa la Kutishia Kuua
Kesi ya kutishia kuua kwa bastola inayomkabili Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe inatarajiwa kuanza kusikilizwa leo.

Shauri hilo lililopo katika Mahakama ya Wilaya ya Iringa linaanza kusikilizwa leo Jumatatu Februari 5,2018 baada ya wiki iliyopita kuelezwa kuwa upelelezi umekamilika.

Katika kesi hiyo namba 189 ya mwaka 2017, Kimbe anadaiwa kutishia kumuua Alphonce Muyinga, ambaye ni katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

Anadaiwa Novemba 26,2017 katika Kata ya Kitwiru ndani ya Manispaa ya Iringa wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwani alitishia kumuua Muyinga kwa bastola kinyume cha sheria.

Shauri hilo linasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi, John Mpitanjia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad