Mfalme wa Saudi Arabia Amewafuta Kazi Mkuu wa Majeshi, Makamanda wa Vyeo vya Juu Jeshini

Mfalme wa Saudi Arabia Amewafuta Kazi  Mkuu wa Majeshi, Makamanda wa Vyeo vya Juu Jeshini
Leo February 27, 2018 habari kutoka nchini Saudi Arabia ni kwamba Mfalme wa nchi hiyo King Salman amefanya mabadiliko katika jeshi la nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwafuta kazi Makamanda wa Vyeo vya juu jeshini akiwemo Mkuu wa majeshi.

Taarifa hiyo imetolewa na shirika rasmi la habari la Saudi Arabia la SPA ambapo limeeleza kuwa Mfalme Salman pia amefanya mabadiliko kwa Makamanda wa vikosi vya nchi kavu na vile vya angani.

Hadi sasa hakuna sababu yoyote ya mabadiliko hayo iliyowekwa wazi lakini inasemekana mabadiliko hayo kiasi flani yameshawishiwa na Mrithi wa Mfalme Mohammed bin Salman.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad