Mfanyakazi Mwingine wa Ikulu ya Trump Aacha Kazi

Mfanyakazi Mwingine wa Ikulu ya Trump Aacha Kazi
Habari kutoka nchini Marekani leo February 10, 2017 ni kuhusu mfanyakazi wa Ikulu ya White house nchini humo ameacha kazi akiwa ni mfanyakazi wa pili kuacha kazi katika kipindi cha wiki moja kwa madai ya unyanyasaji.

Mfanyakazi huyo ambaye alikuwa Mwandishi wa hotuba za Ikulu hiyo David Sorensen ametangaza kuacha kazi baada ya mke wake wa zamani Jessica Corbett kuliambia gazeti Washington Post kwamba Sorensen alikuwa akimnyanyasa kimwili na kihisia katika kipindi chote cha ndoa yao ya miaka miwili na nusu.

Kujiuzulu kwa Sorensen kunakuja siku mbili baada ya Katibu wa Wafanyakazi wa Rais Trump, Rob Porter pia kujiuzulu baada ya wake zake wa zamani wawili kuweka madai ya kuteswa kimwili na kijinsia na Porter.

Sorensen ameeleza kuwa ameamua kujiuzulu ili kwamba Ikulu hiyo isichafuliwe na tuhuma hizo dhidi yake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad