Mgombea CUF Kupeleka Hoja Binafsi Bungeni

MgombeaCUF Kupeleka Hoja Binafsi Bungeni
Mgombea ubunge kupitia chama cha CUF, Rajabu Juma amesema akichaguliwa atapeleka hoja binafsi bungeni kuitaka Serikali itoe angalau mlo mmoja kwa wanafunzi ili watulie shuleni.
Pia alisema akichaguliwa kuwa mbunge ataweka utaratibu maalum wa kuwasajili wafanyabiashara wadogo ili watambulike na wajiwekee akiba yao na yeye kama mbunge wao atawachangia kidogo.
‘’Nikichaguliwa nitashinikiza serikali iongeze maslahi ya walimu ili wasifikirie kufanya biashara ndogondogo badala yake wafundishe kikamilifu’’amesema
Amesema akichaguliwa ataanzisha mfuko maalumu wa bima ya Afya kwa ajili ya wanawake na watoto ili watibiwe kwa gharama nafuu
Mgombea huyo amesema kwamba akiwa mbunge atabainisha maeneo ambayo watachimba visima kwa ajili ya kuwapatia wananchi maji safi na salama.
Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Abdul Kambaya amesema leo watamaliza mkutano wao mapema saa 11:40, kisha wataondoka kwa pamoja kwenda ofisi za chama Fulani kuchukua bendera zao.
Tatizo letu kwenye uchaguzi huu si kumpinga mgombea wa CCM bali kubadilisha mfumo. Na mtu wa kubadilisha mfumo huo ni Rajab Juma.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad