Mke wa Sugu Afunguka Haya Baada ya Sugu Kuhukumiwa Miezi Mitano

Mchumba wa Sugu Afunguka Haya Baada ya Sugu Kuhukumiwa Miezi Mitano
Mchumba wa Mhe. Joseph Mbilinyi “Sugu', Happyness Msonga amefunguka na kusema kuwa kitendo cha kufungwa jela miezi mitano kwa mchumba wake huyo kinaweza kuleta athari kidogo kwenye familia lakini amedai alishajipanga kukabiliana na hali hiyo.


Happyness amesema hayo leo Februari 26, 2018 baada ya Sugu kukutwa na hatia na kushtakiwa kwenda jela miezi mitano na kusema kuwa tayari alianza kupambana na changamoto hizo hivyo haitakuwa na tatizo.

"Pengo ni kubwa kwa sababu Joseph ana familia lakini pia mbali na kuwa Mbunge pia ni mfanyabiashara kwa hiyo utaona changamoto ambazo nitabaki nazo lakini si changamoto kwa sababu nimeshazikabili kipindi ambacho alikuwa ndani kwa mwezi mzima, nilikuwa tayari na familia na kuweza kusimamia kila kitu bila tatizo lolote" alisema Happyness

Mbali na mchumba wa Sugu mke wa Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga, Grace Malya naye amedai kuwa kifungo hicho cha mumewe kitaathiri familia yake na kudai kuwa lakini wao walikuwa wameshajiandaa kwa jambo hilo.

"Hata leo pia hukumu hii sikuipokea sawa sawa na bado ni changamoto lakini hatuna jinsi kwa kuwa tayari wameshaamua japokuwa tulikuwa tunaona dalili zote kwamba hili litatokea" alisema Mke wa Masonga
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad