Mkuu wa Wilaya ya Pangani Amshauri Mumewe Kuoa Mke wa Pili ...... Amuandalia Mavazi ya Kuolea

Mkuu wa Wilaya ya Pangani Amshauri Mumewe Kuoa Mke wa Pili ...... Amuandalia Mavazi ya Kuolea
Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah, ameushangaza umma baada ya kumpongeza mume wake kwa kuongeza mke wa pili, kwani ni kitendo cha nadra sana kwa wanawake kufanya hivyo licha ya kuwa misingi ya dini inaruhusu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mkuu wa wilaya huyo ameandika ujumbe huku akiujulisha umma kuwa wazo la mume wake kuongeza mke wa pili lilitoka kwake, baada ya kuona majukumu ya kazi yanambana na kushindwa kutekeleza majukumu ya ndoa.

“Assalaam Alaykum, nichukue nafasi hii kumpongeza Mume wangu  kwa kuongeza mke wa pili. Kwa kuwa dini yetu ya Kiislam inaruhusu, wazo la kufanya hivyo lilitoka kwangu, kulingana na uzito wa majukumu yangu nalazimika mda mwingi kuwa mbali na nyumbani na hivyo mume wangu kukosa huduma za msingi”, ameandika Bi. Zainab Abdallah.

Mheshimiwa huyo wa serikali ya wamu ya tano aliendelea kuandika kuwa ...”Namshkuru kwa kunielewa na kulifanyia kazi ombi langu, hatimaye nimempata mwenzangu wa kusaidiana naye majukumu mazito ya ulezi wa mume. Alhamdulillah, M/Mungu ametupa riziki na uwezo, hivyo tunapaswa kutumia neema hizi na wengine. Mavazi ya mume wangu nimeyaandaa mwenyewe, yaa rabb atupe stara inshaaAllah.


Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HAO NDO WALEEE WANAWAKE WA PEPONI,,Na inshaallah pepo inamhusu,sema na wewe mtarajiwa husilete HILA Utalaanika hapa DUNIANI...MAISHA MEMA...

    ReplyDelete
  2. majukumu ya kikazi hayawezi kukusababisha kukosa muda na familia yako. hata kama dini inaruhusu. dini haijasema ukiwa na majukumu mengi ndio uruhusu mwenza wako kuoa.labda ishapoteza lengo kwake. wewe kama kiongozi unatwambia kwamba wajiriwa wa kike waruhusu waume zao kuoa kwa sababu ya majukumu ya kazi? au huo ni mfano gani unaotutolea.siafikiani na wewe kwa hilo.matokeo ya ulichokifanya kusingizia majukumu ni kuwafanya wanaume kupoteza dhira ya ndoa sababu tu za wake zao kuajiliwa.i dont support this even if dini inaruhusu.

    ReplyDelete
  3. umejizadhalisha kiongozi nasie wanawake webzio umetudhalilisha sana. zaidi sana naweza sema una yako ni bora ungekaa kimya usiongee I we siri ya nyumbani kwako.

    ReplyDelete
  4. umejizadhalisha kiongozi nasie wanawake webzio umetudhalilisha sana. zaidi sana naweza sema una yako ni bora ungekaa kimya usiongee I we siri ya nyumbani kwako.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad