Msigwa: "Nchi yetu imefika Mahali pa Hovyo"

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (CHADEMA), Peter Msigwa amefunguka na kudai nchi ya Tanzania imefika mahali pa hovyo kutokana na watawala kuiendesha nchi kwa mtazamo wao na sio kufuata sheria na kanuni zilizopo.

Msigwa ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akimuombea ridhaa mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni Salum Mwalimu ili aweze kupata kura za ndio kwa wananchi hao siku ya kupiga kura ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Mhe. Edward Lowassa , huku akisindikizwa na mameya na Wabunge mbalimbali kutoka UKAWA.

"Watawala wanaendesha nchi kwa 'personality' na badala ya sheria na kanuni. Kwa bahati mbaya sana wale ambao wanategemewa kusema, kukemea pamoja na kuonya wamekaa kimya. Lakini baadhi yetu tumeamua iwe mvua, jua, iwe mabomu ya polisi, vituo vya polisi hata gereza tutazungumza hatutoogopa mtu yeyote", alisema Msigwa.

Pamoja na hayo, Msigwa aliendelea kwa kusema "nchi ya Tanzania imefika mahali ambako kiongozi hawezi kusemwa, Mkuu wa Mkoa hata Spika wa Bunge".

Kwa upande mwingine, Msigwa aliwaambia wananchi wa Jimbo la Kinondoni kwamba wakimuona Mbunge anajikomba komba serikalini basi watambue mtu huyo hatambui wajibu wake anaopaswa kuutekeleza au kuufanya.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mbunge gani anaewakilisha wananchi anaejisifia kuwa kinara wa vurugu? Hii ni dalili tosha inayoonesha watu kama Msigwa hawafai kuwa wawakilishi wa wananchi. Kauli za kujigamba kuwa yeye ni mtu wa kupambana na mabomu ni kauli za hovyo na za kijinga. Kiongozi gani anaehamasisha wananchi uvunjifu wa sheria? Siasa sasa imeingiwa na watu wa wapumbavu na hovyo kabisa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad