Msukuma: Lema, Mbowe na Msigwa Wamekuwa Watetezi wa Wezi wa Madini

Msukuma: Lema, Mbowe na Msigwa Wamekuwa Watetezi wa Wezi wa Madini
Mbunge wa Geita Vijijini kwa tiketi ya (CCM) Joseph Kasheku aka Musukuma amefunguka na kusema kuwa yeye licha ya kuishia darasa la saba lakini uwezo wake wa akili ni mkubwa kuliko Mhe. Freeman Mbowe.


Musukuma amesema hayo Februari 11, 2018 aliposhiriki katika kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Kinondoni ambapo alitumia jukwaa hilo kujibu kauli za watu kwenye mitandao ya kijamii wakimtaka asijifananishe na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe ndipo hapo aliposema kuwa akili zake ni zaidi ya kiongozi huyo wa CHADEMA.

"Huko kwenye mitandao wanasema mimi siwezi kujilinganisha na Mbowe nataka niwaambie na mnisikilize mimi nina akili kuliko huyo Mbowe, kwanza mimi ni darasa la saba kama niliweza kuwazungusha wao wenyewe wakakologa nikachomoka bado mimi nitakuwa mjinga" Alihoji

Msukuma aliendelea kusema kuwa wabunge wa upinzania akiwepo Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Peter Msigwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wamekuwa watetezi wa wezi wa madini bungeni. 

"Tukikamata mwizi au tukitumbua jipu linatetewa bungeni na upinzani wale wale waliowaaminisha Watanzania kwamba nchi hii imeibiwa kwa muda mrefu, Msigwa na Lema wamepiga kelele miaka yote toka mimi nikiliangalia bunge wakisema tunaibiwa madini lakini Rais wetu aliposhika madini wakakaa kikao na kuanza kuwatetea bungeni" alisema Msigwa
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Msukuma ni mtu smart sana kuliko Mbowe hilo halina ubishi. Msukuma kama angelikuwa Mwenyekiti wa Chadema CCM ingetaabika sana hilo halina ubishi. watanzania wanashindwa kufahamu yakwamba siasa sio usomi peke yake bali na hekima za kipropaganda alizojaaliwa mtu na Msukuma yupo vizuri. Ila Msukuma anatakiwa kurudi darasani kuongeza elimu yake ya juu ili kuendana na changamoto za wasifu wake kwani uwezo anao kama ataamua kufanya hivyo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad