Mtandao wa Wanafunzi Wamtaka Waziri Mwigulu Nchemba ajiuzulu


Leo February 18, 2018 Mwenyekiti wa mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Abdul Nondo amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kujiuzulu kutokana kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji NIT. Pia kama atashindwa basi Rais amtengue.

“Tunamuomba Waziri wa Mambo ya Ndani, ajiuzulu kwa sababu ameshindwa kusimamia nafasi yake na kuangalia mienendo ya Jeshi la Polisi ambapo kila siku matukio yanatokea,” -Nondo

“Haya matukio yamekuwa yakishamiri sana ambapo yalianzia kwa wanasiasa, ambapo tulikuwa tukiyasikia haya matukio hadi kwa wanafunzi na watu wasiokuwa na hatia,” -Nondo
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Si waziri peke yake. Mkuu wa polisi, mkuu wa mkoa, afisa wa tume ya uchaguzi, na pia tunawataka wanasheria wakuu wa nchi hii kusimamia haki kwa vyama vyote ili jambo kama hili lisitokee tena. Ni viongozi wengi walaumiwe . sheria zisipofanya kazi, watu wanapokaa kimya wakiona wenzao wananyanyaswa. Polisi inapovunja sheria mara m.nyingi kuwashambulia wapinzani.kuwapiga, kufyatua risasi. Ni magunia mangapi ya watu yameokota ufukweni na vyombo vyote vya dola na chama tawala hawalaumu.Ni maovu mangapi yanatendeka hadharani kivyama CCM chama tawala na wasomi chungu mbovu ndani ya chama wako kimya wakishuhudia ualifu mkuu.uchama, uccm, ndio tatizo kuu nchini limewafumba midomo, macho wanaccm na viongozi wengi nchini kuto kutenda haki.watu wote wangeungana kama watanzania kulilia sheria, katiba, haki, kuyakemea mauaji, kulaumu polisi wanapotumia dilaha ovyo na ubabe, huyu binti angekuwa mzima. Sheria zinapopinduliwa matokeo yake ndio haya. Kuuawa kwa watu wasio na hatia. Mmeshuhudia watu kuukotwa ufukweni, lakini watanzania wengi mko kimya, hadiriki kuwatafutia haki hao wasio na sauti sababu hamjaziona picha zao. Wengi ni wazuri kama huyu binti, walikuwa na ndogo zao, na watoto wa mtu, baba au kaka shagazi au mjomba wa wa mtu. Mmekaa kimya bila kupza sauti.mnalea haya mambo ni kama si tatizo la nchi. Hakuna usalama nchini. Wanausama tumeona mara nyingi ni wao wanavunja sheria. Mmeona mkiungana hata raisi analazimishwa kuuona ukweli. Mpaka raia mjue haki zenu , mkiungana kuzidai ndipo mtakapozipata.ni mtanzania kwanza aungwe mkono na si raisi kama ccm ilivyokuja na slogani mpya na kimekuwa chanzo kipya cha ufujaji pesa za watanzania kwa kurudia upigaji kura haramu kwa kuwateka wajinga toka chadema na kuwarudisha ndani ya ccm kwa nguvu. Hili ndilo tatixo kuu lililosababisha huyu binti yetu auwawe . ccm ilimchukua mtu ambaye alishapigiwa kura, wakafosi uchaguzi tena kumpigia huyu huyo avae gwanda rangi yau tu na arudi tena kule kule kwa wananchi wale wale. Kama huu si uchochezi uliobarikiwa na uongozi wa juu wa ccm basi ni nini. Pesa zinazotumika kiujinga katika uongozi huu kurudia uchaguzi. Raisi alishasema nendeni mkafanye kazi mpaka twenty twenty. Ni yeye huyuyu huyu anapanda majukwaani kwa uchaguzi ambao ulishafanyika. Watu haeafikiri hata na kuiona kasoro huu. Uchaguzi ulishapita kwa gharama kubwa sana. Raisi ndiye mwenyewe kupitia chama chake ndiye anayevunja sheria ya kuacha uchaguzi akiruhusu uchaguazi tena kabla ya muda wake kusudi na nia ccm tena . ccm inajiandaa mida hii kwa chaguzi 20wp kabla ya muda wake kupitia majukwaani ikiongozwa na na raisi yuleyule aliyepinga. Kwa sababu wengi ni ccm hawaoni huu uvunjaji wa kisheria. Na wanadheria wetu mizigo sijui kazi zao ni nini au nao wanatimiza na kuunga mkono Ndugu Magufuli. Mwingiliano wa serikali na sheria bila kujitambua au kwa makusudi.Haya ndiyo yanayotuangusha nchini. Zorotesha uchumi. Sababu siasa nyingi.ua watanzania wasio na hatia. Na shetia inshindwa kuwatafuta wahalifu inakuwa ni kawaida na watu hawapo serious. Hata ni kutafuta milo tu. Elimu zetu. Na kudjindwa kufikiri, kuhji mambo, kuwa huru na serious na kuwa wazalendo. Tonarudi nyuma kimaendeleo. Amani inapotoweka basi Taifa linayumba. Hakuna stability ya nchi.
    Kungekuwa na amani safi, basi raisi asingehitaji walinzi twenty four hours. Nyerere alikuweza kutembea bila ulinzi mkali kama sasa. Inamaana kuna kadoro kiusalama nchini. Hii itafutiwe utambuzi mgumu na wakati umefika wa kudai usalama , amanii, utulivu, na ulinzi kwa kila mtanzania sawa.na si viongozi wa juu pekee.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad