Mtanzania Ahukumiwa Jela Ghana Baada ya Kukamatwa na Dawa za Kulevya

Mtanzania Ahukumiwa Jela Ghana Baada ya Kukamatwa na Dawa za Kulevya
MWANAMKE raia wa Tanzania, Basaida Zena Jafary amehukumiwa miaka mitano jela baada ya kukamatwa akiwa na mzigo wa madawa ya kulevya yenye uzito wa Kg 2.3 (Cocaine na Heroine) yanayokadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani 70,000 (zaidi ya Tsh. Milioni 155).

Bi. Zena ambaye ni mfanyabiashara wa chakula akiwa nchini alifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kotoka Ghana (KIA) akitumia Ndege ya Shirika la Rwanda Air yenye namba ET 200 ambapo maofisa hao walibaini shehena hiyo ya dawa hizo haramu zilizowekwa katika bahasha mbili.

Akihojiwa na maofisa hao, alikiri kumiliki bahasha hizo na kukiri kuwa alipewa na Bwana Mandanje Omari raia wa Tanzania na kutakiwa kuzifikisha kwa mtu mmoja anayeishi katika Jiji la Accra.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad